
Mwanamziki wa bongo nchini Tanzania Omary Ally Mwanga maarufu Marioo kwenye tasnia ya muziki ameweka wazi kilichomchochea kumujengea nyumba mama yake mzazi.
Baadhi ya sababu kuu ambayo Marioo ameitaja, iliyomchochea kumujengea mama yake mwanzo ni maisha ambayo waliishi zamani na kumbukumbu hiyo humufika na kuwaza walikopita na mama yao siku za nyuma.
"Kilichonisukuma, unajua siku nyingi tumekaa katika mazingia yasiyo mazuri. Nimeandika kitu kidogo sana kati ya mengi ambayo tuliyapitia. Nakumbuka tulikuwa tunaishi sehemu moja ilikuwa inaitwa Kilalani minazi mirefu, mama yangu alikuwa na chumba kimoja alikuwa analipa ilifu 15 [ za kitanzania ] na mama yangu alikuwa na watoto watatu ambao ni mimi kaka yangu na dada yangu. Tulkuwa tunaishi pamoja hapo," alifichua Mario.
Mwanamziki huyo wa bongo Tanzania pia alieleza kwamba alimpa mama yake nafasi ya kuchagua anapotaka ajengewe na akachagua mwenyewe na anaona amani sana kumufurahisha mama yake.
"Nyumba iko Dar es salaam Mbagala. Mama mwenyewe alichagua na kusema nataka upande huu ili nikitaka kurudi kwa bibi yako inakuwa rahisi. Kweli inakuwa rahisi kuliko kule kule tulikoishi, kumutembelea mama yake. Kwa hivyo nimefurahi kufanikisha hilo swala,' aliweka wazi mwanamziki huyo.
Marioo, ni mwimbaji wa Tanzania, mtunzi wa nyimbo, na mtayarishaji wa muziki. Anajulikana kwa vibao vyake kama vile Bia Tamu, Mama Amina, Dear Ex, Raha, Mi Amor na Naogopa, nyimbo ambazo zimemfanya kutengeneza jina nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Alipokuwa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari aliacha shule na kuhamia Temeke, Dar Es Salaam kuishi na mama yake baada ya kukaa na nyaya yake kwa muda.
Akiwa Dar Es Salaam Marioo alianza kufanya kazi katika karakana ya mjomba wake kama fundi wa magari. Ilikuwa wakati huu ambapo alianza kuandika nyimbo kwa wanamuziki wengine.
Kabla ya kuwa mwimbaji Marioo alianza kama mtunzi wa nyimbo, akitunga nyimbo kwa wasanii wengi. Baadhi ya nyimbo alizotunga Marioo kwa wasanii wengine ni pamoja na Wapo, wimbo wa Mwasiti, Banana wa Dogo Janja, Mchaka Mchaka wa Shilole, Nampa Papa na Gigy Money, Nabembea na Ditto miongoni mwa zingine.
Mwaka 2015 alirekodi wimbo wake wa kwanza, "Dar Kugumu" ambao baada ya kutolewa ulipokelewa vizuri na mashabiki na kuendeleza kipaji cha muziki.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!