Joseph Mayanja alimaarufu Jose chameleon ni msanii wa haiba tena wa viwango vikuu sana katika taasinia ya muziki.
Jose chameleon alizaliwa mnamo tarehe 30 Aprili,1979 Kampala Uganda,katika safari yake ya kimziki Jose chameleon ni msanii wa Kipekee tena wa haiba ya juu kutokana na viwango vyake vya kuimba.
Chameleon ni msanii mwenye kipaji taajika ni msanii ambaye ana uwezo wa kuimba katika lugha ya Kiganda,Kiswahili na Kingereza .
Kutokana na uwezo huu msanii Chameleon ana ufuasi wa mashabiki kote Duniani kutokana na mvuto wa sauti Pamoja na Lahaja yake ya kuvutia.
Aliyekuwa spika wa Bunge la Uganda bi Rebecca Kadaga aliwahi kumpendekeza msanii Jose Chameleon kama balaozi wa masuala ya Utalii sehemu za Busoga,vilevile aliwahi pendekeza wakufu wake wa kuinua na kulea vipaji kwa wanafunzi ambao hawana uwezo wa kujikueza.
Jose Chameleon ni miongoni mwa wasanii wachache ambao hutumia umaarufu na vipaji vyao kuweza kuhamasisha jamii kuhusu masuala yanayoisonga kama vile Maradhi ya ugonjwa wa Ukimwi na kuendeleza kampeni dhidi ya kuhamasisha jamii.
Msanii Jose chameleon alipokea tuzo nyingi katika sanaa hio ya mziki kutoka kwa mashirika mbalimbali, mnamo mwaka wa 2004 alituzwa tuzo ya pearl of Africa music Awards ‘PAM’ kama msanii bora wa Mwaka na wimbo wake wa Jamila.
Tangu mwaka wa 2006 hadi mwaka wa 2018 msanii Jose Chameleon amekuwa akipokea tuzo moja baada ya nyingine mtawalia, Tuzo ya mwisho ni ya mwaka wa 2018 ambayo alituzwa kama bingwa aliyebobea na kukubuhu katika ulingo wa sanaa ya mziki.
Baadhi ya vibao ambavyo bingwa huyu wa mziki amewahi vicharaza ni kama Badilisha,Tubonge,Forever,Valuvalu miongoni mwa vingine vingi vilivyomfanya kuwa kidedea katika Nyanja ya mziki.
Msanii Jose Chameleon ni msanii tena Baba mwenye Familia ambaye ana jumla ya Watoto watano Abba Marcus Mayanja, Ama Christian Mayanja,Alba Shyne Mayanja, Alfa Joseph Mayanja na Ayla Onsea Mayanja.
Kwa sasa mwanamziki huyo maarufu mzawa wa Uganda yuko nchini Marekani kwa ajili ya Matibabu maalum kutokana na ugonjwa wa utumizi mwingi wa Pombe kupita kiasi katika Kongosho yake alimaarufu ‘acute pancreatitis’.
Kwa siku za hivi Karibuni akiwa hospitalini aliweza kurekodi video akisema kuwa kwa sasa hali yake inazidi kuimarika na yuko salama wa salimini.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!