
Michuano ya nusu finali na finali tayari pia imeorodheshwa na tarehe kamili kuwekwa wazi kwa timu husika na mashabiki.
Paris Saint-Germain 'PSG, timu ambayo inafanya vizuri kwa sasa, ilitoa ushindani mkubwa zaidi katika hatua ya 16 bora. Walistahili kuwatoa Liverpool katika mashindano hayo baada ya kuwa timu bora zaidi ya mpira wa miguu katika hatua hiyo.
Aston Villa ndicho kibarua kikubwa kilichoko mbele yao huku Villa wakijaribu kutafuta kuingia katika mechi yao ya nne ya nusu fainali katika kipindi cha miaka 30. Mabingwa hao wa 1982 wanashindana katika hatua hii kwa mara ya kwanza tangu kutetea taji hilo kulipomalizika mikononi mwa Juventus msimu uliofuata.
Nafasi ya robo fainali ya Arsenal ilihakikishwa katika mechi yao ya kwanza ya 16 dhidi ya PSV Eindhoven baada ya kutwaa ushindi wa 7-1.The Gunners wameona changamoto yao ya ubingwa wa Ligi Kuu England ikipanda moshi baada ya kuchapwa kwenye mechi kadhaa hivi karibuni lakini wanapigiwa upatu kwenda Ulaya msimu ujao. Hata hivyo, Real Madrid ni changamoto kubwa sana ili kufikia nusu finali msimu huu.
Barcelona wanaonekana kurudi vizuri sana msimu huu. Wakatalani hao wakiongozwa na mshindi wa 2020 Hansi Flick, wamepita robo fainali mara moja tu tangu ushindi wao wa mwisho mwaka 2015, muongo mmoja uliopita. Benfica hatimaye hawakuwa na mechi rahisi katika hatua ya 16 bora kwa timu hiyo inayoongozwa na Lamine Yamal, Robert Lewandowski na mshindani wa Ballon d'Or Raphinha.
Borussia Dortmund ambao walimaliza wa pili msimu jana 2024, hawana msimu mzuri wa Bundesliga, lakini wameshindi Sporting CP na Lille katika raundi ya mtoano. Hadi sasa wanamiliki mfungaji bora wa pili wa mashindano msimu huu: Serhou Guirassy (mabao 10).
Mwisho miamba wa fainali ya 2010, wakati Inter ya Jose Mourinho ilikamilisha safari ya kihistoria kwa kuwashinda Bayern Munich ya Louis van Gaal huko Bernabeu watakutana tena lakini msimu huu kwa robo finali
Bayern ilithibitisha ushindi mkubwa zaidi, 5-0 kwa jumla, dhidi ya wapinzani wao wa ndani Bayer Leverkusen katika hatua ya 16 bora.
Michuano ya robo finali itachezwa kati ya tarehe 8/9 na marudio 15/16 mwezi aprili.
Paris Saint-Germain Vs Aston Villa
Arsenal Vs Real Madrid
Barcelona Vs Borussia Dortmund
Bayern Munich Vs Inter
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!