
MATOKEO ya historia ya ‘Google search’ kwenye simu ya mtuhumiwa yametumika kama Ushahidi mkuu katika kesi ya mauaji ya mwanamke ambaye alikuwa mpenzi wake.
Ty Vaughn, 31, kutoka jimbo la Texas nchini Marekani sasa anashtakiwa upya kwa mauaji ya mpenziwe baada ya awali uchunguzi wa kifo hicho kuonekana kama wa mtu kujitoa uhai mwenyewe.
Kwa mujibu wa jarida la PEOPLE, Vaughn alikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji mnamo Ijumaa, Machi 7, kuhusiana na mauaji ya Januari ya Luis Banos mwenye umri wa miaka 27.
Mnamo Januari 14, maafisa wa polisi walijibu katika jumba la ghorofa huko Baytown baada ya mpiga simu 911 - ambaye baadaye alitambulika kama Vaughn - kudai kuwa amepata mchumba wake amekufa kutokana na jeraha la risasi, taarifa hiyo inasema.
Ndani, polisi walimkuta Banos akiwa amekufa na jeraha dhahiri la risasi na kumzuilia Vaughn kwa mahojiano.
"Wakati wote wa uchunguzi, Vaughn alitoa taarifa zisizolingana," polisi walidai. "Baadaye wapelelezi walibaini sababu ya kifo kuwa mauaji."
Vaughn sasa anashtakiwa kwa kumpiga risasi Banos usoni na bunduki na baadaye kuonyesha mauaji kama mtu wa kujitoa uhai.
Hii ni baada ya kubainika kwamba alitafuta mtandaoni ili kujua madhara yalikuwaje kwa "raia halali" kumuua "mhamiaji haramu," kabla ya kifo cha Banos, kulingana na waraka huo.
Nyaraka za mahakama zilizotajwa na ABC13 zinasema kwamba polisi waligundua kuwa aliwahi search kwenye mtandao wa Google, "Je, ninaweza kumuua binadamu haramu?"
Kulingana na Fox 26, nyaraka za mahakama zinaonyesha Vaughn baadaye aliwaambia polisi kwamba mchumba wake "hakuwa na hadhi ya kisheria."
Polisi wanadai Vaughn alikuwa anajaribu "kupunguza au kudharau hadhi au thamani ya (Banos')," kwa kujadili hali yake ya uhamiaji, ripoti za San Antonio Express-News, zikinukuu hati ya kiapo ya upekuzi. Banos aliripotiwa kuwa mzaliwa wa Mexico.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!