Mmiliki Mwenye hisa za asilimia kubwa ndani ya timu ya kandanda ya Manchester United Inayoshiriki Ligii kuu ya Uingereza EPL Sir Jim Ratcliffe  amefichuwa kwamba wanaweka mipango kabambe ili kuhakikisha wanatwaa kombe la ligii ya EPL ndani ya miaka Mitatu.

Akizungumza kwenye mahojiano na mwanahabari wa BBC ameeleza kwamba licha ya wakati mgumu ambao wanapitia kama timu  kwa sasa bado wanatia bidii kubadilisha hali hiyo. Mmiliki huyo pia ameelelza kwamba watakuwa wanaadhimisha miaka 150 ya timu hiyo ifikiapo mwaka 2028.

"Kuweka ratiba ni sawa. Ni wazi kuwa ni maadhimisho ya miaka 150 ya kile ninachofikiri ni klabu kubwa zaidi duniani ya mpira wa miguu mnamo 2028 kwa hivyo nadhani ni lengo nzuri sana. Ikiwa hiyo inawezekana...  Sina uchawi . Siwezi kuona katika siku za usoni, bila shaka,' alieleza.

Mkufunzi huyo amelinganisha changamoto zao na zile walizopitia wapinzani wao kwenye ligii hiyo kama Livepool na Arsenal katika misimu michache iliyopita.

"Nadhani ukiangalia Arsenal, ukiangalia Liverpool, ukiangalia kipindi ambacho kiliwachukua kupanga nyumba kwa utaratibu na kurudi kwenye njia za kushinda... Lakini haiwezekani. Naangalia Liverpool wakati Klopp alipowasili mwaka 2015 akiwa na Michael Edwards na Ian Graham kwa upande wa data, walijenga upya kikosi hicho zaidi ya 2015, 2016, 2017 na 2018 na kisha wakashinda kila kitu mwaka 2019, 2020 na 2021,"aliendelea.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mikel Arteta amekuwa Arsenal kwa miaka minne au mitano sasa, na unaweza kuona Arsenal iko katika nafasi tofauti sana na ilivyokuwa miaka mitano iliyopita. Kwa hiyo, nadhani tunazungumza juu ya miaka mitatu. Labda hiyo ni kabambe kidogo lakini nadhani ni maadhimisho ya miaka 150 kwa hivyo ni lengo nzuri kwetu. Tuko hapa. Tunapaswa kujipima wenyewe. Kama tunafanya mambo ambayo tulisema tutafanya ambayo ni kuirudisha United mahali ambapo inapaswa kuwa," alisema mmiliki huyo.

Wakati huo alionekana kutofurahishwa na msimamo wao katika jedwali ambao wanashikilia nafasi ya 14 na alama 36 nyuma ya viongozi wa Ligii vijana wa Arne Slot Liverpool. Hata hivyo amesema kwamba sasa ni wakati wa mabadiliko na mambo yatakuwa sawa.

"Ni wazi kwamba sio mahali ambapo tunataka kuwa, lakini tuko katika kipindi cha mabadiliko. Hatujapata muda mwingi wa kubadili kikosi, tuna kocha mpya ambaye alikuja katikati ya msimu, na tuna orodha ndefu ya majeruhi," alieleza

'Ukiangalia wachezaji wanane wa juu katika Manchester United, Ruben [Amorim] ana wanne tu kati ya hao kwa sababu wengine wanne hawapatikani kwake. Kwa hiyo nikiangalia kikosi ambacho kinapatikana kwa Ruben, nadhani anafanya kazi nzuri ya kuwa mkweli," alifafanua.