Mwanamziki Gift Stanford Joshua maarufu Gigy Money kutokea katika taifa la Tanzania ameweka wazi kwamba wakati utafika na atamurudia Mwenyezi Mungu.

Msanii huyo wa Bongo alikuwa akielezea baada ya video yake kusambaa na Irene Uwoya huku akieleza kwamba uwoya anajaribu kumueleza amurudie Mwenyezi Mungu.

"Mungu, nataka nijisifie jina lake, Kama naweza kufanya wasichana wote mkanunua vipini mkatoboa pua, mkanunua mawigi ya kigeni, mbona sio hili la kumusifu Mungu. Mbona sio kumusifu Mungu, mimi ikifika wakati wa kuthubu dhambi zangu nithatubu. Ikifika Muda Mungu atanipeleka," alifunguka mwanamziki Gigy.

Msani huyo pia alikariri kwamba Uwoya amekuwa akimusihi sana athubu dhambi zake na kumurudia Mungu. Jambo ambalo ameeleza kwamba ikifika muda mwafaka wa kufanya hivyo atathubu.

Mimi mara nyingi naongea na Irine mtumishi wa Mungu, hata ikifikia mahali atake kuwa prophet ataweza sababu anamusikia Mungu sirini na anampa ujumbe mtu mwingine," Alieleza

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"Mtu kama mimi amenisumbua karibu miaka mitatu akiniambia Gigy nimekuota tena, Gigy Mungu anakuita, Gigy njoo umutumikie Mungu. wakati mwingine unawezachukulia kama kiki kaka. Ukachukulia kama huyu naye ana shobo huyu ananidanganya,' alieleza msani huyo kuhusu jitizaada za Uwoya Kumurai kuokoka.

Gigy pia amefunguka kwamba amejifunza kutoayatilia maanani baadhi ya mawaidha ya watu wengine amabao wanamtaka aache kumusikiliza Mtumishi Uwoya kutokana na histora yake ya zamani huku akiwaeleza kwamba kwa sasa Uwoya alibadilika.

"Wengine wanaendelea kunishauri kwamba Irine anataka tu mkajiuze, jamani alibadilika, Irine tuliyemjua yule wa madibao mnamuona sai, kwani mnafikiri yale maisha ni rahisi sana au magumu sana, nakwambia ni shetani tu umemkaribisha," alisema msani huyo.

 Gigy alipata umaarufu baada ya kuachia Papa, wimbo wa Bongo Flava uliotungwa na Marioo mwaka 2017. Katika kazi yake ya muziki, Gigy Money amefanya kazi mbalimbali ya muziki ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Whozu, Tamimu, Rosa Ree, Lava Lava na zaidi.

Mwanamuziki huyo  mara kwa mara ametuhumiwa, kushtakiwa na wakati mwingine kupigwa marufuku kwa kukiuka utaratibu wa uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini Tanzania.