Mwimbaji Feza Tadei Kessy ameibua madai kwamba Msemaji wa timu ya Yanga inayoshiriki ligi kuu nchini Tanzania amekuwa akimsumbua mara kwa mara kwa kumutumia jumbe za kumtongoza.
Mrembo Feza Kessy alieleza haya wakati akizungumza na mtangazaji Mwijaku huku akichukua hatua zaidi kumuonesha jumbe zenyewe kwenye simu yake alizotumiwa na Ali Kamwe.
Ali Kwame Kabla ya Hapo alikuwa amepinga kwamba tangu apewe namba na mwanadada huyo hajawahi kumutafuta hata kwenye simu.
Mwanadada Kessy hivi maajuzi alieleza kwamba hawezi kuolewa na Ali Kamwe Kisa tofauti za imani katika dini huku akisisitiza kwamba yeye ni mkiristu mwenye imani sana na amezaliwa mara ya pili na Ali Kamwe ni wa dini ya kiislamu hivyo hawaendani.
"Ally Kamwe kiukweli aliniomba namba, ushikaji wetu ulianzia pale kwa Hamisa. Sio kitu kibaya mimi kumpa namba, kitu kilichoko hapo ni kwamba yeye sio Mkiristu na mimi sio Muislamu... Watu wengi wanafikiria mimi ni Muislamu labda kwa sababu ya jina langu lakini mimi si Muislamu. Mimi ni Mukristu ambaye nimezaliwa upya," mrembo Kessy alisema hapo awali kuhusu swala la kuolewa na Ali Kamwe.
Mwimbaji huyo pia alieleza kwamba hajatupilia mbali swala la kuwa kwenye mahusiano na Ally Kamwe, ila kutoka na tofauti ya imani zao ndizo changamoto kubwa. Alieleza kwamba kwake yeye hayuko tayari kubadilisha dili ila akasema yuko sawa iwapo Ali atabadili na hapo atakuwa tayari kuanzisha mazungumzo.
"Hata akija nitasema hapana kubwa, 'akiamua kubadilisha' hilo litakuwa sawa na sasa hapo ndio maongezi yataanza. Hamna kitu kibaya kuingia kwenye urafiki hasa urafiki wa kuowana na mtu kisha vitu haviendani," alieleza Feza AWALI KIDOGO.
Feza alianza kazi yake kama mwanamitindo na mrembo wa zamani, mwaka 2005 alitawazwa kuwa Miss Dar City Centre, Miss Ilala na Miss Tanzania Mshindi wa pili akiwa na umri wa miaka 17.
Feza aliachia wimbo wake wa kwanza, Amani ya Moyo, mwaka 2013, baadaye akatoa My Papa, wimbo ambao ulimfanya kuwa miongoni mwa wanamuziki wanaokuja kwa kasi.
Mnamo 2021 Feza alitia saini mkataba wake mkubwa zaidi alipotangazwa kuwa msanii wa kwanza wa kike wa 'DB Records' lebo ya rekodi inayomilikiwa na nyota wa Nigeria Oladapo Daniel Oyebanjo, anayejulikana zaidi kwa jina lake la kisanii D'banj. Feza alitoa wimbo wake wa kwanza Bless Me kwenye DB Records.[
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!