Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga ametangaza rasmi kuhusisha chama chake moja kwa moja na serikali ya Kenya Kwanza inayoongozwa na rais Williama  Ruto katikia mkutano wao uliofanyika katika jumba la mikutano la KICC.

Odinga ambaye amekuwa mzoefu kwenye Tasinia ya siasa ya miungano na Marais walioko serikalini kwa muda murefi ametangaza kushirikiana na serikali ya rais Ruto na Naibu wake Profesa Kithure Kindiki.

Kiongozi huyo wa chama cha ODM ameanza na kuzungumzia safari yaka na maamuzi ya kuamua kushindania nafasi ya kuwa mwenyekiti wa tume ya umojja wa Afrika AU.

Raila alieleza kwamba aliombwa na viongozi wakubwa Africa ili awanie nafasi hio kama mtu ambaye alikuwa anaelewa mambo ya kiafrika vizuri hivyo wakamutuma aliyekuwa rais wa Nigeria Obasanjo kuleta ripoti.

"Nilitafutwa na viongozi wakubwa hapa Afrika, walipoona kwamba nafasi hio itaachwea wazi walihitaji mtu ambaye anaelewa Afrika vizuri ili aende ajaribu kuleta lengo lao pamoja ambalo baba zetu wanizilishi walikuwa nalo...Wakamutuma rais wa zamani wa Nigeria,  Obasanjo aje aniombe niwanie nafasi hiyo... na rais Ruto akaja kunisaidi jambo ambalo sikutarajia.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Odinga alieleza kwamba licha juhudi zote matokeo hayakwenda vizuri na baada ya kurudi nyumbani walimutaka asaidie serikali kufanyia wakenya.

'Nliporudi nilienda kukutana na rais huko Mombasa  ili kumushukuru kwa kunisaidia wakati wa kampeni...nilipata pande zote mbili zimepanga na walitaka niweke sahihi tushirikiane pamoja lakini nilioma muda nifanye mashauriano kwa watu wetu na nilifanya hivyo," alisema Odinga.

"Tuko hapa kufanyia Pamoja kama ODM na UDA ili kusaidia kuendeleza taifa..ili tuweze kutatua mambo ya kibiashara, uchumi na siasa ambayo watu wetu wanaqpigana nayo.  Sisi kama viongozi wa vyama vikuu ichini tumekubaliana kwamba wakati kuna changamoto katika taifa hatufai kukaa nje na kuendelea kuwakejeli. Tusaidiane kuendesha taifa, kutumia vyama vyetu kama njia ya kuifikia sauti za watu," alieleza waziri mkuu huyo wa zamani.

Mwanasiasa huyo hata hivyo ameeleza kwamba kushirikiana kwao hakuhusishi kuunganisha vyama vya kisiasa badala yake kusongesha taifa mbele.

" Kwa muungano huu wa MOU tunakubaliana kushikilia Katiba, sheria zilizopo na kuheshimu haki za kila binadamu. Tunaahidi kushugulikia swala la ukosefu wa ajira, mzigo wa maisha, kupigana na umasikini, kupigania usawa na kurejesha matumaini kwa wizara ambazo zimeathirika na ufisadi," alieleza.

"Tunaahidi kutetea ugatuzi ili kusaidi kuinua uchumi sehemu zote za taifa. tutakuwa tunapeleka mswada kwamba hakuna kaunti ambayo itapokea chini ya billioni 450 kwa mwaka, Mwisho tunaweka wazi kwamba Memo ambayo tumeweka sahihi leo haihusu muungano wa vyama kati ya ODM na na UDA , lakini ni kwa sababu ya mwendelezo mzuri wa taifa letu siku za baadaye,'" mwanasiasa huyo alikamilisha.