
KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Ijumaa, Machi 7, 2025.
Katika taarifa ya Alhamisi jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Nandi, Kakamega, Vihiga, Tharaka Nithi.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mtaa wa Kilimani zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Sarwat, Tachasis, na Meteitei katika kaunti ya Nandi zitakosa umeme kati ya saa tatu unusu na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Chimoi na Lwandeti katika kaunti ya Kakamega yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Vihiga, sehemu za maeneo ya Ebwali na Waluka zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Kariakomo na Keria katika kaunti ya Tharaka Nithi pia zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!