Mtoaji motisha mmoja huko Tanzania anayejulikana kama Chief Godlove sasa anasema kwamba sio lazima usikilize kila kitu ambacho mzazi anasema. Anaeleza kwamba ni vyema wakati mwingine kuwapuuza wazazi iwapo unahisi mawaidha yao sio ya muhimu kwa wakati huo.
Godlove amesisitiza kwamba mtu binafsi ndie hujua mipango yake kwa maisha na wala sio mzazi. Kwa hivyo ni vyema kufanya maamuzi yako ya kipekee ili usije ukamulaumu mzazi kukupa uwamuzi usio sahihi hasa kwenye maswala ya kibinafsi kama kutafuta utajiri.
"Mzazi wangu mimi hajawai kuwa tajiri na hajui kitu chochote kuhusu utajiri, ananishauri vipi kuhusu utajiri. ananiambia soma uwe tajiri, lima uwe tajiri. Ananiambiaje hiki fanya, hiki usifanye, yeye hakufanya ndo maana hana. Unajua vijana wengi tumeaminishwa na wazazi wetu kwamba mtu ukishakuwa tajiri uowe," alisema Godlove.
"Sasa kuna sisi ambao hatujengi tunanunua. Yaani mimi nikiona nyumba umejenga umemaliza nanunua nyumba yako nanunua na gari. Wazazi pia na wao sio watu wa kuwasikiliza sana," alendelea.
Mtoaji Motisha huyo alifichua kwamba yeye wazazi wake walimtaka aoe mapema baada ya kuwanza kupata vihela vidogovidogo. Ameongeza kwamba kama hangefanya uwamuzi wake mzuri angefeli katika maisha.Mtoaji Motisha huyo alifichua kwamba yeye wazazi wake walimtaka aoe mapema baada ya kuwanza kupata vihela vidogovidogo. Ameongeza kwamba kama hangefanya uwamuzi wake mzuri angefeli katika maisha.
Kama mimi hapa, ningewasikiliza wazazi wangu mpaka leo ningekwa nimefeli. Walinilazimisha nioe wakati amba nimetoka kumaliza kidato cha nne. kuna bint mmoja alionekana eti ana akili akili mtaani wazazi wangu wakaanza kumulazimisha nimuoe yule binti. Kwa sababu nilikuwa naonekana nina maisha angalau tofauti na wale vijana wengine. Ningeoa ningepotea ndio maana nasema pia kila muda sio wa kuwasikiliza wazazi.
Mtoaji Motisha huyo ameeleza kwamba sasa hivi amefanikiwa na ana pesa na uwezo wa kununu taifa kama vile Kenya.
'Hela nilizo nazo nanunua Kenya nzima ile , yaani Nairobin Mombasa,Naivasha, Kilimani, Kakamega nanunua hizo zote,' alijigamba
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!