
KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Machi 5.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti kumi za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Machakos, Nakuru, Nandi, Kakamega, Tharaka Nithi, Nyeri, Kiambu, Kitui, na Kilifi.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Mbagathi Way, Umoja 1, Tena na Umoja Innercore zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na mbili jioni.
Sehemu za Athi River katika kaunti ya Machakos zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa nane alasiri.
Sehemu za Northsore-Naivasha katika kaunti ya Nakuru zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Eneo la Cheptabach katika kaunti ya Nandi zitaathirika kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Eneo la Bukhakunga Sihome katika kaunti ya Kakamega litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Tharaka Nithi, sehemu za maeneo ya Mwanjanje na Kathanga zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.
Mji wa Kiriani katika kaunti ya Nyeri utaathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Raiyani, Kahunguini na Nembu katika kaunti ya Embu yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Wakati huohuo, maeneo ya Iganga, Mbitini, na Voo katika kaunti ya Kitui pia yataathirika.
Sehemu za maeneo ya Mwango, Mtondia, na Tezo pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!