Mshambuliaji wa pembeni wa Chelsea inayoshiriki ligii kuu ya uingereza 'EPL' Mykhailo Mudryk sasa amefunguka kwamba amepoteza watu wa familia wapatao watano kwenye mapigano ambayo yanaendelea nchini mwao Ukraine kati ya taifa hilo na taifa jirani la Urusi.
Mchezaji huyo wa taifa la Ukraine kwa sasa anaandamwa na sheria na mashirikisho ya michezo ya huko ulaya kwa madai ya kutumia dawa za kuongeza nguvu ambazo zilipigwa marufuku kwa wanariadha na wanakandanda wote.
Mchezaji huyo alieleza haya wakati akijaribu kuweka wazi kwamba yeye yuko safi na wala hajatumia dawa hizo ambazo ni haramu. ameeleza kwamba amepoteza matumain katika maisha.
Kulingana na yeye ameeleza kwamba baada ya kuwapotezaxc wanafamilia kitu peke kilichobaki kumpa tumaini kilikuwa mpira lakini kwa sasa pia amesimamishwa kujishughulisha na mchezo huo uchunguzi ukiiendelea kufanyika.
"Nimepoteza watu tano wa familia katika vita tangu uvamizi wa Ukraine. Sasa kitu pekee ambacho kilinifanya nifurahi kimeondolewa kutoka kwangu. Nimeachiwa nini? Ni vigumu sana kuwa katika hali hii, nimesema kuwa sina hatia na bado ninasimama nayo. Ninawasihi kila mmoja kuwa mtulivu, ukweli lazima utoke siku moja na nawashukuru nyote kwa ujumbe." alisema Mudryk.
Mhezaji huyo kwa sasa ameondolewa miongoni mwa wachezaji wanaoshiriki ligii zote za timu hio. Ila riporti haijaweka wazi iwapo anaendelea kufanya mazoezi na kikosi cha timu hiyo.
Mnamo 2023, alihamia klabu ya Uingereza Chelsea katika uhamisho wa thamani ya awali € 70 milioni (£ 62 milioni), na kumfanya kuwa mchezaji wa bei ghali zaidi wa Ukraine na mchezaji ghali zaidi aliyesajiliwa kutoka Ligi Kuu ya Ukraine.
Mudryk amekuwa mchezaji wa kimataifa wa taifa la ukreni tangu 2022, baada ya hapo awali kushiriki katika viwango kadhaa vya vijana. Aliwakilisha timu hiyo katika UEFA Euro 2024.
Mnamo Desemba 2024, Mudryk alishindwa mtihani wa dawa zilizopigwa marufuku na alisimamishwa kwa muda kutoka kwa mpira wa miguu. Sampuli yake ya pili ya mkojo bado haijachunguzwa.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!