Makao makuu ya papa mjini Vatica yamesema kwamba Papa Francis aliendelea kuwa imara siku nzima ya Jumapili na hakuhitaji tena matumizi ya mashine ya kupumua.
Vatican ilisema hayo wakati wa maelezo kuhusu maendeleo ya Papa huyo mwenye umri wa miaka 88 wakati akiendelea kupambana na homa ya mapafu.
Papa Francis amekuwa katika hospitali ya Gemelli mjini Rome kwa zaidi ya wiki mbili. Alilazwa Februari 14 akiwa na maambukizi makali ya kupumua ambayo yalisababisha matatizo mengine.
Taarifa hiyo ilisema kuwa Papa hakuwa na homa siku ya Jumapili. Ila madaktari walikuwa wanaendela kujitahidi kumlinda hasa kutoka na picha za X- rays ambazo zinaonesha kwamba Papa bado hajaondoka hatarini.
Vatica imesema kwamba Papa hakuhitaji tena matumizi ya kile ambacho Vatican imekiita "non-invasive mechanical ventilation" lakini alikuwa akiendelea kupokea oksijeni kupitia bomba dogo chini ya pua yake.
Papa Francis alipata matatizo ya kupumua siku ya Ijumaa, sawa na shambulio la pumu, jambo ambalo lililazimu awekwe kwenye Mashini ya kumusaidia kupumua hata hivyo Vatican ilisema kwamba hali ya Papa ilikuwa imetuliakutokana na tatizo hilo.
Papa Francis ambaye alikutana mapema Jumapili na maafisa wawili wa Vatican na alitioa shukrani kwa waombezi kwa sala zao na msaada wao katika ujumbe ambao ulikuwa umeandikwa.
Ningependa kuwashukuru kwa maombi," alisema Papa Francis katika barua iliyotolewa na Vatican kwenye eneo la sala yake ya kawaida ya Jumapili na mahujaji, ambayo Papa hakuweza kuongoza kwa wiki ya tatu.
"Ninahisi upendo wenu wote na ukaribu wenu... Ninahisi kana kwamba 'nimebebwa' na kuungwa mkono na watu wote wa Mungu," ujumbe huo ulisema.
Papa Francis pia alikutana hospitalini siku ya Jumapili na Kardinali Pietro Parolin, afisa nambari mbili wa Vatican na naibu wa Parolin, amesema msemaji wa Vatican Matteo Bruni, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu kiini cha mkutano huo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!