John Philip Ouma alimaarufu msanii Madini Classic ni msanii wa Bongo Mkenya mzaliwa wa Kisumu.
Alizaliwa mnamo Desemba 2,1994 katika gatuzi la Kisumu mkoa wa Nyanza Japo aligura na Kwenda nchi ya Tanzania wakati ambapo kipaji chake cha usanii kilichipuka.
Baada ya muda Madini alirudi nchini Kenya na kuka upande wa Pwani,alianza safari yake ya usanii akiwa mdogo alipokuwa akijifunza kuimba miziki aina ya bongo.
Katika hali yake ya udogo na ujana Madini alikuwa akiimba na kurekodi nyimbo kadhaa ila alikosa mtaji wa kurekodi video akawa ametulia chini ya zulia akisubiri hali imwendee nyema kihela.
Madini classic alipagazwa jina MADINI kutoka kwa babu yake aliyekuwa anafanya kazi nchii ya Tanzania ambaye alikuwa mchimba migodi mahiri na madini kule Taifa la Tanzania.
Katika safari yake ya muziki madini classic alivicharaza vibao kadha ambavyo vilimkweza na kumuweka katika safu ya wasanii bora ukanda wa Afrika Mashariki na Kati hadi upande wa janga la Sahara na baadhi ya sehemu za Mto Limpopo.
Baadhi ya Vibao ambavyo Madini ameviachilia ni Nitalewa,Taratibu,Goma,Toto la Kanairo,Bingo Bango,Tawire miongoni mwa vibao mbalimbali ambavyo vilihanikiza na kuteka anga kwa mirindimo ya kipekee.
Katika mahojiano na kituo cha Habari cha Mpasho Madini aliwahi sema na kusadiki kuwa mara nyingi yeye huwa hapendi kuishi maisha ya bandia ili ifahamike na watu kuwa hali yake ya Maisha i sawa kumbe la.
Madini alielelezea kuwa katika safari yake ya muziki na maisha yake kwa jumla hajawahi kuazia kujihusisha na maisha ya kughushi katika hali halisi ya hapa duniani yeye hukiri na kususia lile ambalo anahisi haliko sawa ila si kufurahisha umma jinsi wasani wengi kwa asilimia kubwa wanavyofanya.
Madini kutokana na mujibu wa maelezo yake alisema kuwa mara nyingi wasanii wengi huwa na hulka ya kutaka sifa na majitapo na kutaka kujulikanaa hivyo kuishia kufanya vitu ambavyo ni kinaya cha kuogofya na uhalisia wa maisha yao.
Kulingana na kujitambua huko kwa Madini ndiko kumempa jina kubwa jina ambalo limejulikana na kupata umaarufu wa hali ya juu sana.
Msanii Madini Classic unaposikiliza vibao vyake utagundua kuwa ni msanii ambaye amezamia kwa lugha ya Kiswahili sanifu yeye ni msanii ambaye ni mtunzi mzuri wa Mashairi ambayo huwa na ujumbe kwa jamii katika viwango vyote si elimu, kilimo ,biashara,siasa na mapenzi ujumbe huwa huwa umekolea sana.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!