kplc

Kampuni ya Kusambaza umeme nchini (KPLC) imetangaza kuwa kutakuwa na katizo la umeme katika kaunti tano siku ya Ijumaa ili kuruhusu matengenezo ya kawaida ya mifumo ya usambazaji umeme.

Maeneo yatakayoathirika yatakumbwa na changamoto za umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti zitakazoatharika ni Nairobi, Kisii, Murang’a, Meru, na Taita Taveta.

Nairobi

Baadhi ya Sehemu za Nairobi zitakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo yaliyoathirika ni Nyangumi Road, Chaka Road, Lenana Road, Turbo Road, Rose Avenue, Jabavu Road, Kasuku Road, Makuyu Lane, Theta Lane, na maeneo jirani.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kisii

Katika Kaunti ya Kisii, umeme utakatizwa kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Maeneo yatakayoathirika ni Nyamaiya, Nyabera, Riagumo, Arura, Gesabakwa, Ekona, Suguta, Nyamondo ATC, Mogenda, Monianku Secondary School, Metaburo Secondary School, Muma Secondary School, Ochodororo Weighbridge, Moticho, na wateja wa karibu.

Murang’a

Wakazi wa Murang’a watakumbwa na ukosefu wa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tano jioni. Sehemu zilizoathirika ni Githambo Market, Kanyenyaini Market, Rwathia Secondary, Rwathia Market, Kiairathe Secondary, Kiairathe Market, Kiawambogo Market, na wateja wa karibu.

Meru

Katika Kaunti ya Meru, umeme utakatwa kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Maeneo yaliyoathirika ni Meru Water Supply, Start Times Network, Katheri, Githogo Town, Githogo T/Fact, Chief Ikunyua, Kirongine, Patmos, Kathumbi, Kainginyo, Kianthumbi, Kithioro, Nthimbiri, Mworoga, Kithaku, Kanthuni, Kathiranga Secondary School, Muringa TBC, Meru Central Dairy Cooling Centre, Githongo Law Courts, Krugwa Girls, Kinjo Market, Hydro PSP, na wateja wa karibu.

Taita Taveta

Katika Kaunti ya Taita Taveta, umeme utakatizwa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika maeneo yafuatayo: Jora, Bungule, Kasigau Girls School, Makwasinyi, na maeneo ya karibu.

Kenya Power inawashauri wakazi wa maeneo yaliyoathirika kupanga shughuli zao mapema na kuomba radhi kwa usumbufu wowote utakaosababishwa na kazi ya matengenezo.