Mwanamziki Feza Tadei Kessy afichua kwamba kwa vyovyote vile hawezi kuolewa na muumini wa dini ya kiislamu. Mwanadada huyo alikuwa akizungumza na wanahabari kuhusu video ambayo imekuwa ikisambaa inayomuhusu yeye na mtoto wa kiume Ally Kamwe.

Kwenye video mwanadada anaonekana akimpa nambari ya simu Ally Kamwe walipokutana kwenye harusi ya Hamisa Mobetto na Aziz.

Ally Shaban Kamwe ni afisa wa habari wa klabu ya mpira wa miguu  (Yanga) iliyoko Tanzania.  anajihusisha na kuendeleza mawasiliano na kutangaza habari muhimu zinazohusu klabu hiyo.

"Ally Kamwe kiukweli aliniomba namba, ushikaji wetu ulianzia pale kwa Hamisi. Sio kitu kibaya mimi kumpa namba, kitu kilichoko hapo ni kwamba yeye sio mkiristu na mimi sio muislamu... Watu wengi wanafikiria mimi ni muislamu labda kwa sababu ya jin langu lakini mimi si muislamu. Mimi ni mukristu ambaye nimezaliwa upya.

Feza pia ameeleza kwamba hajatupilia mbali swala la kuwa kwenye mahusiano na Ally Kamwe, ila kutoka na tofauti ya imani zao ndizo changamoto kubwa. Ameeleza kwamba kwake yeye hayuko tayari kubadilisha dili ila akasema yuko sawa iwapo Ali atabadili na hapo atakuwa tayari kuanzisha mazungumzo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"Hata akija nitasema hapana kubwa, 'akiamua kubadilisha' hilo litakuwa sawa na sasa hapo ndio maongezi yataanza. Hamna kitu kibaya kuingia kwenye urafiki hasa urafiki wa kuowana na mtu kisha vitu haviendani,"  alieleza Feza.

Hata hivyo mwimbaji huyo wa Bongo amesisitiza kwamba anahitaji muda zaidi ili kuingia katika mapenzi mengine, ila hajaeleza kilichomfika kwenye mapenzi yake ya awali.

Kulikuwepo na fununu kwemba yuko kwenye mahusiano na mwanamziki Harmonize  baada ya kiongozi huyo wa Konde gang kupost picha yake, wote wawili hakuna aliyethibithisha hilo.

"Kuheal, nimeshaheal lakini kufungua moyo wangu kwa mtu mwingine itachukua muda, mwanaume kunibadilisha mawazo kwamba nimpe nafasi," Kessy alifunguka.

Feza ni mzaliwa wa jijini Nairobi Kenya na amekukulia hapa nchini na wazazi ambao walikuwa wenye asili ya Kitanzania na anatoka katika familia ya watoto wa nne

Feza alianza kazi yake kama mwanamitindo, ni mrembo wa zamani, mwaka 2005, alitawazwa kuwa Miss Dar City Centre, Miss Ilala na Miss Tanzania Mshindi wa pili akiwa na umri wa miaka 17.

Feza aliachia wimbo wake wa kwanza, Amani ya Moyo, mwaka 2013, baadaye akatoa My Papa, wimbo ambao ulimfanya kuwa miongoni mwa wanamuziki wanaokuja kwa kasi.