Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ametabiri kwamba Erling Haaland atarudi kutoka kwenye jeraha la goti "Hivi karibuni" na bado ana matumaini kwamba mshambuliaji wa klabu hiyo anaweza kucheza dhidi ya Tottenham Hotspur siku ya Jumatano.

Haaland amekosekana katika mechi mbili za mwisho za City. Baada ya kuwatazama wachezaji wenzake wakisambaratishwa na Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki iliyopita kama mchezaji mbadala ambaye hakutumika, Haaland hakuwa hata kwenye kikosi cha City kwa kipigo cha mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili.

Raia huyo wa Norway amekuwa akiuguza jeraha la goti alilopata wakati wa mchuano baina ya timu yake  dhidi ya Newcastle United tarehe 15 Februari.

Kocha huyo wa Catalan alifichua kuwa jeraha hilo "si hatari", jambo ambalo ni faraja kwa mashabiki. "Uchunguzi wote unaeleza kuwa ni sawa, lakini hakujisikia vizuri," Guardiola alielezea.

"Nina hisia kwamba [kurejea kwa Haaland] itakuwa hivi karibuni, kwa sababu jana tulifanya mazoezi na alifanya vizuri sana. Lakini alisema hakuwa tayari, na tunapaswa kuheshimu hilo. Ni matumaini yangu kuwa katika michezo ijayo anaweza kutusaidia."

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

City itasafiri kuelekea uwanja wa Tottenham Hotspur Jumatano usiku, uwanja ambao Guardiola amepoteza mechi sita kati ya nane. Alipoulizwa kama Haaland atapatikana kwa safari hiyo ijayo, alisema: "Kuna matumaini."

"Kwa kweli, tutamkosa," Guardiola aliongeza. "Katika kipindi cha miaka tisa iliyopita, tulicheza mechi nyingi bila wachezaji muhimu na tulinusurika. Msimu huu tumekuwa na majeraha mengi lakini hatukuweza kusitahimili.

Katika misimu yake miwili na nusu huko Manchester City, Haaland amekosa mechi 26 tu katika mashindano yote. Nyingi ya mechi hizo zilikuwa za upinzani wa ligi ya chini katika vikombe vya ndani, i City bado imeshinda zaidi ya asilimia 73% ya michezo ambayo Haaland amekosa katika misimu iliopita.

Spurs haijawa na uwezo wa kujilinda msimu huu, lakini wanafurahia ushindi wa muda mrefu zaidi katika ligi nzima, huku wakiwa na ushindi wa tatu mfululizo wa Ligi Kuu England kabla ya ziara ya City katikati mwa wiki.

Kwa sasa Manchester City ya Pep Guardiola inashikilia nafasi ya 4 wakiwa nyuma ya Liverpool, Arsenal na Nottingham forest mtawalia huku wakifatiwa kwa karibu na Newcastle.