Mike Mbuvi Sonko, gavana wa zamani wa Nairobi amelalamika kuhusu hali ya uchumi  baada ya kuishiwa na mafuta kwenye gari lake katika barabara ya Kiambu. 

Sonko alitaja 'uchumi mbaya' kuwa changamoto kwa watu wa matabaka yote. Alisema kwamba ni jambo la kawaida kuishiwa na mafuta wakati huu kulingana na uchumi uliopo.

"Hii economy ni mbaya, mbaya kabisa, yaani Sonko mzima anaishiwa na mafuta bwana, hapa Kiambu road, mimi naendesha gari naishiwa na mafuta bwana," gavana huyo wa zamani wa kaunti ya Nairobi alilalamika.

Hata hivyo baada ya muda mchache aliletewa mafuta kwenye mtungi huku akionesha aibu kwa kuishiwa mafuta barabarani kisha kuletewa mtungini.

"Inaitwa economy, Sonkoree anaweka mafuta na kibuyu, hali ni ngumu majamaa. Hawa jamaa wameniletea mafuta ni waoga hawataki wajulikane wameniletea mafuta kwa kibuyu, hii ni hali ya kawaida bwana, economy ni mbaya,'" alisema mwanasiasa huyo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Sonko kwenye video tofauti baada ya muda mchache alionesha akiwekewa  mafuta kwa gari lake yenye kiasi cha shilingi elfu 11. baada ya gari kujaa.

"Weka elfu kumi na tano, 15 thousand, super," alisema. "God's time is the best." 

Mwanasiasa huyo alionekana mwenye furaha baada ya kulijaza gari lake mafuta, na kuwatania waliokuwepo kwamba walimukata kuwa kiongozi wao Nairobi.

"Mlinikataa kuwaongoza," alisema.

Hata hivyo wenyeji wa hapo walijitenga na madai hayo na kumuomba arudi wakati mwingine.

"Sisi hatukukataa, tunakupenda, rudi mara ya pili," mwenyeji mmoja alisema, huku wengine wakimpongeza kwa kumchukuwa yule mtoto wa chekechea na kuishi na yeye baada ya baba yeke kuuliwa kwa kisu na watu wasiojulikana.

Sonko alimushangaza muhudumu wa stesheni hiyo ya Mafuta baada ya kumpa kibunda cha pesa ahesabu mwenyewe atowe kiasi chake kisha arejeshe inayobaki.

"Kuja, toa hapa, pesa ngapi nimekunywa, toa hapa elfu kumi na moja alafu unirejeshee zingine," alisema baada ya kumpa bunda la pesa muhudumu.

Mike Sonko aliongoza kaunti ya Nairobi kama gavana wa pili baada ya kuchukuwa usukani kutoka kwa mtangulizi wake Evans Kidero. Hata hivyo aliondolewa mamlakani na bunge la kaunti hiyo baadaa ya madai ya kuhusika na ufisadi na kutoheshimu ofisi ya gavana.