
Kizaaza kilishuhudiwa jijini Nairobi inje ya makao makuu ya Kenya Power baada ya usimamizi wa kaunti ya Nairobi kumwaka taka mbele ya ofisi zao.
Duru zinaarifu kwamba mgogoro kati ya serikali ya kaunti ya Nairobi na ofisi ya huduma za Kenya Power umekuwepo kwa muda mrefu sasa anavyoeelza msimamizi.
'Tumekuwa na mgogo mrefu na kaunti ya Nairobi kuhusiana na swala la kulipia bills zao. Sisi tunafanya kazi yetu na majukumuu yetu ni kupena umeme, na matarajio yetu ni kwamba baada ya kuduma wateja wetu wanafaa kulipa. '
Wasimamizi wa ofisi za Kenya Power wamesema kwamba walikuwa wakiendelea na shughuli zao za kawaida kabla ya magari ya kumwaga taka ya serikali ya kaunti ya Nairobi kufikaka na kumwaga taka.
"Asubuhi ya leo tulikuwa tunaendelea na kazi zetu kaqma kawaida, kisha tukaona magari ya serrikali ya kaunti ya Nairobi ambayo yanabeba taka, na gari moja likakuja moja kwa moja na kumwaga taka hapa mbele ya ofisi yetu ya kushughulikia maswala ya pesa, Stima Plaza. Pia kuna magari mengime ambayo yako karibu hapa.
Ofisi ya kenya power pia Imweripoti kukatiwa maji na serikali ya kaunti hiyo ya Nairobi. Na hilo sio tu kwa hii ofisi pekee yake lakini kwa ofisi zetu zingine zilizoko hapa Nairobi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!