
MWANASOSHOLAITI Vera Sidika ameonyesha kutoridhishwa kwake na huduma ya ukandaji ambayo alifanyiwa akwa nchini Marekani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Ijumaa, Sidika alilalamika akisema kwamba alifanyiwa masaji katika eneo moja nchini Marekani na licha ya kulipishwa kiasi kikubwa cha fedha, hakuridhia na huduma hiyo.
Sidika alionesha risiti ya malipo kwa huduma ya kukandwa – shilingi 42,000 pesa za Kenya ambapo baadae aligundua kuwa huduma ya kukandwa haikumridhisha.
“Masaji hii ilinigharimu shilingi 42,000 pekee lakini kusema kweli ilikuwa duni zaidi. Sasa nahitaji masaji nyingine ili kupona kutonana na hii,” Vera Sidika alichapisha.

Sidika ambaye amekuwa akichapisha picha akizuru Maeneo mbalimbali ya haiba ya kipekee nchini Marekani alionekana kupendelea huduma za kukandwa ambazo anapata humu nchini.
Wiki chache zilizopita, sosholaiti Vera Sidika alichapisha picha zake akila kwenye mkahawa mmoja na kuonesha pesa taslimu na risiti ya pesa nyingi.
Sidika anajulikana kwa maisha yake ya kifahari na ameonekana akionyesha mavazi ya wabunifu, likizo za kifahari, na mali za kifahari.
Katika chapisho moja, alishiriki kwamba alikuwa ametoka kwa chakula cha mchana na akaeleza kwa utani chakula hicho kama "chakula cha Kenya" anachokipenda zaidi.
Katika chapisho jingine, alionyesha risiti ya mlo wa jioni uliogharimu KSh 198,000.
Onyesho la Sidika lilivuta hisia na mashabiki walimiminika mitandao ya kijamii kwa hisia. Wengine walihoji ikiwa onyesho lake lilikuwa la kufurahisha au kujionyesha bila madhara.
Sidika alipata umaarufu mwaka wa 2012 aliposhirikishwa katika wimbo wa P-Unit "You Guy". Mnamo 2014, alionekana katika single ya Prezzo, "My Gal".
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!