Mbwana Yusuf Kilungi alimaarufu Mbosso ni mwanamziki kutoka Tanzania alizaliwa Kibiti mwambao wa pwani mnamo Oktoba 3,1995.
Mbosso ni mtoto wa Yusufu Mbwana Kilungi na Khadija Salum Kikali wazazi ambao walikuwa wakifanya kazi za kijungu jiko ili kujikimu kimaisha,baba alikuwa akifanya kazi ya Utingo huku mama akifanya kazi ya ukulima.
Mbosso katika utoto wake alikuwa mtoto mwerevu aliyependa masomo na kutunga nyimbo na kuziimba,aliazimia kusoma zaidi ila kutokana na hali ngumu ya maisha na kipato kidogo cha familia Mbosso alisoma hadi kidato cha nne.
Alipofika kidato cha nne na ikapatikana kuwa hamna hela za kumuwezesha kuendelea na masomo aliwarai wazazi wake wampee kibali afuate nyota yake ya talanta,Wazazi waliwazia ombi lake kisha wakamruhusu afuate azima yake kama msanii.
Katika safari yake ya Maisha Mbosso alionekana kidedea na mchangamfu sana ka kila hatua aliopiga ilizaa matunda.
Baada ya Mbosso kuwaza sana ni wapi atakapoanzisha maisha yake upya aliamua kugura nyumbani na kuenda Dar salaam kuenda kutingiza kibiriti kuona kama ndani mna njiti.
Alipofika Dar es Saalam alikumbana na ugumu wa hali ya maisha akawa na hali tete kimawazo alipokuwa katika shughuli zake za hapa na pale alikutana na mkubwa na wanawe ambaye alimshika mkono na kumshirikisha katika bendi iliyovuma sana ya Yamoto Bendi.
Akijiunga na bendi hiyo ya Yamoto bendi ambayo iliwashirikisha vijana wenzake wenye vipawa angavu kama chake waliweza kuimba nyimbo ambazo zilikuja zikavutia mashabiki na kuwa kipenzi cha wengi nchini Tanzania na ukanda wa Afrika mashariki kwa jumla.
Mbosso alikuwa na wasanii wenzake kwa jina Aslay ,Beka Flavour na Enock Bella waliovuma 2018 na kuwa mahiri wakubwa na kuonyesha ushuja na ubunifu wa hali ya juu sana.
Baadhi ya Vibao ambavyo mbosso alivicharaza baada ya bendi yao maalum Yamoto bendi kuvunjika na hatimaye akajisajili na lebo ya Wasafi rekodi Sambapo aling’ara zaidi baadhi ya Vibao alivyovicharaza ni Nadekezwa,Hodari,Watakubali miongoni mwa vingine vingi zaidi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!