mwanamume mwenye babymamas 7

MWANAMUME ambaye anajipiga kifua kwa kuwa na familia pana yenye wake halali wawili na wanawake wengine 5 ambao amezalisha nje ya ndoa amedai kwamba yuko tayari kuendeleza msururu wake wa kuzalisha wanawake tofauti tofauti.

Mwanamume huyo mwenye umri wa makamo alikiri hayo wakati alipotokea kwenye mahojiano ya runinga.

Alisema kwamba yeye hupata tulizo la moyo katika kumpa mwanamke mimba pindi anapohisi kuwa na msongo wa mawazo kutokana na mahusiano na wanawake wengine.

“Mimi nina wanawake wawili, pia nimezaa nje na wanawake 5 hivyo kwa jumla nina watoto 7 kutoka kwa wanawake 7. Na katika hawa wanawake wangu wawili, mmoja ni mzungu mwingine ni mwafrika. Na wote tumeoana kwa njia halali kabisa kwa neema ya Mungu,” Mwanamume huyo alieleza kwa majigambo tumbi nzima.

“Sasa, sharti nambari moja katika nyumba yangu ni kwamba kama watanipa msongo wa mawazo kupita kiasi hiyo inamaanisha ni lazima nitoke nitafute mwanamke mwingine, kwa sababu naamini ninaishi mara moja tu!” aliongeza.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans
×

Video hiyo ambayo ilichapishwa kwenye ukurasa wa Facebook kwa jina 9ja Now ilivutia maoni mseto, baadhi wakimuunga mkono kwa dhana kwamba anafurahia maisha yake duniani huku wengine wakidai kwamba alikuwa anawachezea wanawake shere.

Wengine pia walimkosoa kwa kurasmisha uchepukaji katika ndoa kuonekana kama jambo la kawaida licha ya kuwepo kwa magonjwa ya zinaa mengi.

@Victoria Anene: Unaweza kufikiria. Mwanaume huyu anadhani anawafanyia wanawake upendeleo.

@Paul Mgbameh: Wewe ni mtu asiyewajibika sana.