Baada ya mwanadada mrembo Rita kuweka video kwenye mitando ya kijamii zikimuonesha yeye pamoja na mwanamziki Diamond Platinumz wakiwa kwenye mahaba, Diamond mwenyewe amesema video hizo ni za zamani.
Huenda Diamond alifanya hivyo kulinda mahusiano yake na mpenzi wake wa sasa Zuchu yasitiwe doa ikiwa kwamba kuna mipango ya wao kufunga ndoa hivi Karibuni.
Ugomvi wa Mrembo Rita na Diamond umechukua mkondo mpya baada ya Mwanadada huyo kuchapisha ujumbe kwenye mtandao wake wa Instagram akieleza kilichomfanya amuache Diamond huku akimtaka msanii huyo kuacha uwongo na aeleze ukweli kilichotokea Katika mahusiano yao.
Mwanadada huyo alisema kwamba ni yeye aliamua kumuacha Diamond platinumz baada ya kugundua kwamba huenda mwanamziki huyo alikua akimuharibia muda tu.
"Mtu unaenikataza nisifanye kazi yoyote nikae tu ndani video call 24/7 af matumizi ya manati unaleta sababu Mia kidogo ukiambiwa kodi ndio kabisa unakimbia kama sio wewe ulienipangia iyo nyumba umecheza na akili yangu sana wewe na ndio tabia yako kucheza na akili ya mwanamke aliekupenda," alieleza
Mrembo huyo alikanusha kwamba rais huyo wa wasafi aliachana naye mwaka 2023 kwan huo ndio mwaka ambao mpenzi wa Diamond Zuchu alikuja kugundua kuhusu uhusiano wao.
"2023 ipi?? Labda unaongelea mwaka ambao msichana wako aligundua tupo pamoja hivo ukasugest tuwasiliane kwa number nyingine ili ajue tumeachana, mimi nmekuacha 2024 November, baada ya Kuona Kisaikoloiia ndipo nikaamua kukutumia hiyo sms ya kukuacha baada yakugoma kulipa kodi." alikanusha madai ya Diamod
Mwanadada huyo pia aliendelea kudai kwamba Mpenziwe wa zamani Diamond alikuwa akimuacha chumbani na kwenda kujivinjari na wanawake wengine.
"Lakini nashukuru Mungu nilistuka mapema wewe mtu mkubwa na pesa bieberi nishinda ukitumia ivo vigezo lakin ukweli unaujua umeninyanyasa sana tumeenda south Unalalala na mwanamke mwingine chumba kingine ambaye ni fantana mi unaniacha chumbani kısa nipo piriod af nakuuliza why umefanya ivo unanigeuzia kibao," alifafanua mrembo huyo.
Madai haya yamewafanya Mashabiki wa Mond kutilia shaka Mahusiano Kati yake na mpenziwe wa sasa Zuchu ambae tayari wametangaza kwamba wanapanga kufunga ndoa. Wengi wakisema kwamba huenda kilichompata Mrembo Rita kikampata mwanamziki Zuchu.
Kwa upande wake Simba la Masimba alikiri kwa uhusiano huo ulikuwepo ila ulikuwa umekatika zamani mwaka 2023. Pia akimutaja mwanamke huyo kuwa muongo na anamharibia jina na hata kuongeza kwamba jambo hilo amelifikisha katika mamlaka husika na taratibu za sheria zitafatwa.
"Nimeona kuna clip zinasambazwa mtandaoni zinazonihusu... clip hizo ni za zamani, mwaka 2023, na zina zaidi ya miaka miwili nyuma. Na mwanamke huyo niliachana na yeye takriban miaka miwili sasa... Lakini pia nilimweleza mwenzangu nilienaye na tukasameheana na tukaanza maisha mapya. Mwanamke huyo sasa ameamua kutumia clip hizo na kuambatanisha na jumbe za uongo kwa lengo la kunblackmail na kutengeneza fedha , jambo hili limeshafikishwa katika mamlaka husika na taratibu za kisheria zinafuatwa. Shukran," Diamond alikamilisha ujumbe wake.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!