Abba Marcus na babake Jose Chameleone

ABBA Marcus, mwanawe msanii nguli wa muda mrefu kutoka Uganda, Jose Chameleone ameibuka tena na mashambulizi makali dhidi ya babake, saa chache baada ya taarifa za msanii huyo kutakiwa kufanyiwa matibabu ya kina kuibuka.


Kupitia ukurasa wa X, Marcus alifoka vikali alimlaani babake na kumuita ‘Baba mbaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya dunia’ wakati ambapo Chameleone anaelekea kufanyiwa upasuaji wa kongosho.


"I have the one of the one of the worse father in the history of the world ?" alichapisha, kabla ya kushiriki machapisho kadhaa akielezea kufadhaika kwake.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


Hii si mara ya kwanza kwa Marcus kumkosoa babake hadharani.


Matamshi yake ya hivi punde yanaonekana kutokana na kisa cha hivi majuzi ambapo Chameleone alikimbizwa hospitalini lakini akachagua kuzungumzia uvumi wa uongo kumhusu kwenye video ya moja kwa moja ya TikTok kabla ya kuzungumza na watoto wake.


"Chameleone a ho... alikimbizwa hospitalini na jambo la kwanza analofanya badala ya kuwasiliana na watoto wake, anaendesha TikTok live lol ???" alichapisha Marcus, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Chameleone na Daniella Atim.


Kijana huyo amekuwa akimshambulia babake mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii, zaidi ya miezi miwili sasa tangu alipolazwa.


“Sifanyi hivi ili kufichua hulka za huyo mtu, ningeweza kuzembea kuanika hovyo hovyo. Yeyote mwenye akili anajua yeye ni nani. Niko kwenye jukwaa LANGU nikijieleza kwa sababu mtandao wa kijamii ni wa kujieleza,’ alijitetea katika moja ya machapisho yake.