
MSANII Stevo Simple Boy amevunja kimya chake baada ya aliyekuwa mlezi wa wanawe Diana Marua na Bahati, Irene Nekesa kumfungulia moyo kwamba anampenda.
Nekesa katika video moja ambayo ilionekana mitandaoni, alikiri penzi lake kudondokea kwa msanii huyo ambaye sasa ni mmiliki mpya wa gari jijini, aina ya Mazda Demio.
Katika video hiyo, Nekesa alijimwaya akimwambia Stevo Simple Boy kwamba yeye ndiye anayemfaa, haswa baada ya Stevo kutendwa katika mapenzi kwa mipigo kadhaa.
Nekesa aliweka wazi kwamba alikuwa chini ya shinikizo kwa penzi la Stevo Simple Boy haswa baada ya kumuona akiwa na gari hilo jipya.
“Acha niseme ukweli, mimi niko na presha, Stevo Simple Boy amenunua gari na hana bibi. Stevo Simle Boy nakutafuta, uko wapi? Nipigie simu, mimi sitaki kujua gari hilo linaitwa aje, ninachokuambia ni kwamba mimi niko single na wewe pia hauna mtu,” Irene Nekesa alisema.
“Nioe angalau ukilia hapo umepiga magoti nakupangusa machozi. Niko hapa, unataka nikuje nikuoshe miguu, nikupanguse nikufanyiwe masaji, niko hapa kwa ajili yako, uko wapi?” Nekesa aliongeza akisisitiza kwamba moyo wake unadunda kwake Simple Boy.
Hata hivyo, Stevo Simple Boy alionekana kutotongozeka na maneno hayo matamu ya Nekesa akisema kuwa anaelewa vizuri kauli hizo alizozitaja kama ‘mchezo wa taoni’.
“Mchezo wa taoni tunaujua vizuri sana,’ Stevo alijibu huku akiambatanisha jibu lake na emoji za kucheka.
Mapema wiki hii, Stevo Simple Boy alifichua kupokezwa zawadi ya gari jipya aina ya Mazda Demio kutoka kwa muuzaji mmoja wa magari humu nchini.
Akitambulisha zawadi yake jipya kwa mashabiki wake mitandaoni, Stevo Simple Boy alionekana amepiga magoti akisujudu kwa furaha ya kuwa mmiliki wa gari jijini Nairobi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!