Anne Kansiime na mpenzi wake, Skylanta

MCHEKESHAJI maarufu kutoka Uganda, Anne Kansiime amezua tetesi za kuvunjika kwa ndoa yake na mumewe, msanii Skylanta.

Fununu za kuvunjika kwa ndoa ya wawili hao ziliibuka mitandaoni baada ya Kansiime kuchapisha ujumbe wa kudai kukosewa heshima.

“Siku moja mtu ambaye ulijitolea sana kwake atakugeuka na kusema hakukuomba ujitoe mhanga kwa ajili yake. Na hili litakuuma kwa sababu atakuwac amesema ukweli. Na hilo limenitokea mimi, licha ya hayo, bado tunasonga mbele na mapenzi lazima yapendwe. Mimi ndiye mapenzi, leo hii ninaanza ukurasa mpya,” Kaansime alichapisha kwenye kurasa zake mitandaoni.

Habari za kuachana kwao zilichochewa zaidi baada ya mumewe kutoa wimbo kwa jina ‘Ex’ ambapo amemtaja mhusika kuwa “mtu asiye na makalio na mwenye kichwa kidogo”.

Wanamtandao wachache wanadai kwamba amekuwa akipitia wakati mgumu katika uhusiano wake na Skylanta na kwamba inaweza kuwa mwishowe mbaya.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Wengine, hata hivyo, wanadai kwamba "zama mpya" anayodokeza katika chapisho la siri ni onyesho lake lijalo la "Comedy Grill" linalotazamiwa kufanyika tarehe 9 Mei 2025.

Kansiime amepokea uungwaji mkono kutoka kwa mastaa kadhaa wanaoendelea kusambaza maneno ya kutia moyo kwenye post yake ya Instagram.

Wawili hao wamekuwa pamoja kwa muda sasa na mnamo Aprili 2021, Kansiime na Skylanta walibarikiwa na mtoto wao wa kwanza, Sellasie Ataho.

Miezi miwili baadae – June, Skylanta alimchumbia rasmi Kansiime na kumvisha pete ya uchumba.

Hata hivyo, haijulikana kama ni kweli wanaelekea kuachana au kuna tatizo kwenye ndoa yao ama ni kiki tu kuelekea shoo yake ya mwezi Mei.