
MTENGENEZA Maudhui ya mitandaoni, Terence Creative amesimulia jinsi umaskini ulikuwa umemzungira na maisha yake lakini maisha yake yakaja kubadilika ghafla.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Terence Creative alichapisha video ambayo alikuwa anakariri shairi kuhusu umaskini enzi hizo.
“Ninaenda kuwakariria shairi lenye mada, Bwana Umaskini…Nimepita tu kusema hi, nina bahati kwamba sijafa kwa sababu yako. Lakini ni nani mwenyeji wako? Ama ulitokea tu kama mzimu na kujikita katika nchi yangu kama bosi bila kutuarifu mwenyeji wako ni nani?...” Terence alikariri shairi lake kwa sehemu.
Alisimulia maisha yake ya awali akisema kwamba haamini jinsi Mungu alimkomboa kutoka katika lindi la umaskini akisema kwamba muda wote Mungu amekuwa naye na kila kitu anamiliki ni kwa neema kutoka kwa Mungu.
“Niliwahi kuwa uso wa umaskini, Mungu alibadilisha simulizi yangu??Mungu ameziongoza hatua zangu siku zote, Alikuwa nami katika siku zangu zilizopita, Yuko nami katika maisha yangu ya sasa na anashikilia maisha yangu yajayo,Nina deni kwa Mungu,” alisema.
Terence Creative ni mmoja kati ya watu maarufu wachache ambao hawaogopi kusimulia maisha yao ya utotoni.
Katika simulizi la awali, Terence alihadithia jinsi alikulia katika maisha yenye taabu na nyanya yake katika mtaa wa mabanda wa Mathare.
Alisimulia kwamba alikuwa ni mtumizi wa sigara lakini aliacha na miezi kadhaa iliyopita, alisherehekea miaka 7 ya kutotumia kilevi hicho.
Leo nina shukrani kwa safari—kila hatua, changamoto, na ushindi umeunda mimi nilivyo leo. Hapa ni kukumbatia njia iliyo mbele kwa mikono miwili, ," sehemu ya maelezo mafupi ilisoma.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!