
HITMAKER wa ‘African Queen’, 2Face Idibia ambaye amekuwa kwenye midomo ya watumizi wengi wa mitandao ya kijamii kwa takribani mwezi mmoja sasa, ameripotiwa kutoweka.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka nchini kwao Nigeria, familia ya msanii huyo ambaye pia anajiita 2Baba ilitangaza kutoweka kwake bila taarifa ya aliko.
Taarifa hii inajiri ikiwa ni siku mbili tu baada ya kumchumbia mpenzi mpya, mwanasiasa Natasha Osawaru.
Mnamo Februari 14, 2025, familia, kupitia kwa mawakili wao, ilichapisha ombi lao la kuingilia kati kutoka kwa Idara ya Huduma za Jimbo, wakitafuta usaidizi wao katika kumtafuta mwimbaji huyo mkongwe.
Ombi hilo lilisomeka kwa sehemu, "Tunaandika ili kuomba usaidizi wako kwa dharura kuhusu hali ya kutatanisha inayohusisha mwanafamilia wa Idibia, Bw. Innocent Idibia (anayejulikana pia kama Tuface au 2Baba), ambaye wateja wetu wanaamini kuwa huenda hayupo tangu Jumatatu 10, Februari 2025."
"Ni muhtasari wetu kwamba Bw. Innocent aliondoka nyumbani kwake asubuhi ya tarehe 10 Februari 2024 akiwa amevalia vazi lake la mapumziko, akidokeza kwamba alikuwa akiendelea na matembezi yake ya kawaida lakini hakurudi nyumbani tangu wakati huo."
Mapema siku hiyo, mnamo Februari 14, 2025, mamake 2Baba alienda kwenye mitandao ya kijamii na kumwonya mchumba mpya wa mwimbaji huyo Natasha Osawaru amwache.
“Akina mama wote wanapaswa kunisaidia kuomba kumsihi Bi Natasha Osawar kumwachilia mwanangu,” alisema kwa sehemu.
Taarifa za kupotea kwa 2Baba ziliwashtua wengi kwani siku moja kabla ya video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ya msanii huyo wa ‘African Queen’ akimtaka mbunge huyo kukubali ombi lake la ndoa mbele ya marafiki zao.
Akiwa amezidiwa na pendekezo hilo, Natasha anaonekana akifunika uso wake kabla ya kusema ndiyo, jambo lililoibua shangwe kutoka kwa mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 49 ambaye kisha akatangaza, "the ayes have it".
Katika video ambayo iliibuka mtandaoni, mwimbaji huyo alimtaja Natasha kama "mwanamke mchanga, mwenye kipaji na mzuri" ambaye alikuwa akitaka kuoana naye. Aliongeza kuwa hakuwa na maswala yoyote na Annie, huku pia akilenga mashambulizi mepesi kwa wakosoaji wake katika wiki zilizopita.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!