Usuli na historia ya msanii Hussein Machozi.

Hussein Rashid Juma alimaarufu Husein Machozi alizaliwa mnamo tarehe 6 Oktoba,1986 Manyoni Singida Tanzania.

Hussein Machozi ni mwanamuziki vilevile ni mtunzi wa nyimbo za kisanaa,Hussein alianza kuimba akiwa  mwana mdogo alikuwa akimwimbia mama yake huku akimuarifu kuwa  ipo siku atakuwa msaanii taajika.

Alipofika umri wa  ujana Hussein alianza kujihusisha katika makongamano na warsha mbalimbali za muziki huku akiwatumbuiza wageni na watu mbalimbali,alizidi kikinoa makali kipaji chake kwa kuendelea kuandika nyimbo na kujituma zaidi.

Kipaji chake kilipozidi kutamba na kung’aa zaidi  Hussein alitambulika nchini Tanzania na kuanza kuimba kwa mvuto wa hali ya juu na akawa anawavutia mashabiki wengi nchini na hata katika mataifa ya Nje kama Kenya na Uganda.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Nyota yake iling’aa pale alipokutana na wanamziki wa bendi ya Sauti Sol na akashirikiana nao na kutoa kibao cha Utapenda kibao mbacho kiliteka angaa na kuwavutia mashabiki wengi,wimbo ambao aliujumuisha katika alibamu yake ya kwanza.

Hatimaya alitoa kibao kimoja kwa jina ‘’Kafia Ghetto’’kibao ambacho kilihanikiza ukanda wa Afrika Mashariki kwa jumla na kummegea sifa belele,kibao hicho kiliweza kuchezwa katika idhaa za Redio Tanzania.

Husein Machozi Kutokana na mtindo wake wa kuimba na kughani mashairi kwa namna ya kipekee ulimpevusha na kumweka katika Daraja ya magwiji wa sanaa ya muziki, hadi leo yeye ni msanii mzuri  tena wa kuigwa katika taasinia ya mziki kwa kuimba vibao motomoto tena aina ya Bongo fleva.

Hussein aliwahi toa vibao vingi vikiwemo kwa Ajili yako,Nipe sikuachi,Full Shangwe,Addicted ,Unanifa, za Mwizi 40 na Jela kibao ambacho kilisisimua umma na mashabiki wake kutokana na utunzi imara na ubunifu wa hali ya juu.

Kibao heri nirudi Jela kilikuwa miongoni mwa vibao ambavyo vilifanya vyema zaidi katika alibamu ya  msanii Husseni na kumpandisha kisanaa, hivyo akawa ni mwanamziki ambaye aliyetambulika na kuheshimiwa sana.

Hussein Machozi kwa muda mrefu amekuwa kimya lakini kutokana na mashabiki wake kushikwa na uchu wa kutaka kumuona akichemka tena na kuachilia magoma ya kipekee wameshinda wakimchokoza wakisema kuwa wangependa kusikia kibao kipya mwaka huu.

Kulingana na dalili za bwana Hussein katika mitandao ya Kijamii japo hajadokeza ni lini ataachilia bonge la kibao kipya ila ameonyesha dalili za kuwajibu mashabiki wake kuwa wawe na Subira mambo mazuri yaja.