Landlord vs Tenant

WATU wengi katika Maeneo ya mjini wanaishi katika nyumba za kupanga, zingine zikisimamiwa na mawakala huku zingine zikisimamiwa na wenye nyumba halisi.

Katika nyumba hizi za kupanga, aghalabu wapangaji hupata masuala kadhaa ambayo wangependa kurekebishwa au kukarabatiwa na wenye nyumba ili kukidhi mahitaji yao haswa katika huduma za muhimu kama maji na umeme.

Sasa mpangaji mmoja amesimulia kisa cha kushangaza jinsi yeye na wapangaji wenzake wamekuwa wakipitia wakati mgumu kumshurutisha mwenye nyumba wao kuwafanyia ukarabati wa baadhi ya huduma katika nyumba wanazoishi.

Kupitia ukurasa wake katika mitandao wa X, mpangaji huyo alisema kwamba yeye na wapangaji wenzake wanaishi katika nyumba zinazomilikiwa na kijana mwenye umri wa miaka 24.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kijana huyo mwenye bahati ya kumiliki mali isiyohamishika ni mtengeneza maudhui wa mitandao ya kijamii ambaye kulingana na mpangaji huyu, amekuwa akiwashikia shokoa kujisajili kwa akaunti zake mitandaoni kabla ya kuwashughulikia mahitaji yao.

Mpangaji huyo alilalamika kwamba kila mara wanapomfuata kijana huyo mwenye nyumba wanazoishi wakimtaka kukarabati baadhi ya vitu, yeye huwashrutisha kwanza kujisajili kwenye Instagram na YouTube zake kabla ya huduma.

“Mwenye nyumba wangu ana umri wa miaka 24. Ukimfikia na malalamishi kuhusu nyumba yako - tuseme, paa inayovuja - atakuambia umfollow kwenye Instagram na YouTube kabla hajafanya chochote," mpangaji aliandika.

Landlord

Aliendelea na tukio lingine ambapo mwenye nyumba aliacha gumzo la kikundi cha WhatsApp kwa wapangaji baada ya mtu kujibu kwa "???" katika kuchanganyikiwa kwa taarifa.

Mwenye nyumba huyo anadaiwa alipata kutoheshimu na akaondoka kwenye kundi hilo dakika tano tu baada ya kujumuishwa.

"Wakati mmoja, aliongezwa kwenye gumzo la kikundi ili aone jinsi tulivyokuwa tunapanga kununua dizeli kwa pampu ya maji. Aliondoka baada ya dakika tano kwa sababu kuna mtu alisema kitu ambacho aliona ni matusi. Ajabu ni kwamba mara nyingi hutumia ‘???’ katika mazungumzo, hata na wakili wake,” mpangaji aliongeza.