
ALIYEKUWA msanii wa Gengetone, Peter Miracle Baby amefichua kwa nini hawezi rudi tena katika uimbaji na utunzi wa mirindimo hiyo.
Akizungumza kwenye podcasti ya Nguthii, Miracle Baby alisema kwamba Gengetone ilikuwa inaelekea kuua vijana na kusema kwamba yeye kama mmoja wa hao vijana, hawezi rudi katika ‘mauti’ hayo.
Miracle Baby alisema kwamba kwa sasa yeye atasalia tu katika kuimba muziki wa Mugithi na kueneza injili, akitabiri Gengetone iliyofufuka kufariki tena kabla mwaka huu kuisha.
“Gengetone ilikuwa inaenda kumaliza vijana, ilikuwa inauwa watu, hivyo mimi siwezi rudi kwa kitu chenye kilikuwa kiniue,” Miracle Baby alisema.
“Gengetone ilikuja kisha ikaisha, hivyo huwezi niambie nirudi kwa kitu chenye kilikuja na kisha kikaisha. Sikudanganyi, Gengetone haimalizi huu mwaka, haiwezi rudia. Hivyo kama hatutakuja na mkakati mwingine sioni kama kuna maana yoyote tunafanya katika hii sanaa,” aliongeza.
“Hatuwezi ishi place moja, baana joo tunazidi kuzeeka ..izo doba ziachiwe up coming wajijenge vile tu zilitujenga tusipo do ivo tutaishi na millions of views bt kwa mfuko zero...for now acha ni pige gospel mugithi zangu.”
Msanii huyo alisema kwamba Gengetone ilikuwa inatumia lugha chafu na haiwezi kudumu kwa muda mrefu kwa sababu watu waliokuwa wanaipenda kipindi kile sasa hivi wameshakomaa kiakili na hawataki tena kusikiliza kwa lugha chafu ambayo ilikuwa inatumika kwenye miziki hiyo.
“Vijana wenye tulikuwa tunaimbia Gengetone kitambo sasa hivi ni watu wako na familia wanatafuta kazi. Hao sasa si wenye tutakuwa tunaimbia, hao watataka tuwaambie vitu vya kupata kazi, venye watapata pesa. Lakini ukisema niimbe tena kuhusu makalio ina maana ninarudi kuimbia tena wenye wako kidato cha 4 sasa, hapo sasa nitakuwa naenda mbele ama narudi nyuma?” Miracle Baby alijieleza.
Miracle Baby alisema kwamba hadhira ya Gengetone ambayo ilikuwa inapenda miziki ya kuzungumzia makalio na viuno vya wanawake sasa ni watu wazima wanataka kusikiliza michongo ya kusaka hela na Imani ya kuishi kuiona kesho.
“Sasa hivi nimeamua kukwama kwa Mugithi na pia kama nitaimba hizo zingine haitakuwa Genge, nitakuja na muziki wangu kivyangu, muziki yenye mtu anaeza sikiliza impe motisha kwa maisha,” alisema.
Hii hapa video akizungumza;
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!