
MWANAHARAKATI na mwanasiasa Morara Kebaso amepigwa na butwaa baada ya kupata jeneza dogo likiwa limetelekezwa nje ya lango la kuingia kwake.
Mwanzilishi huyo wa chama cha INJECT alichapisha video kwenye ukurasa wake wa X akilikagua jeneza hilo dogo.
Baada ya kulifungua jeneza hilo, Kebaso alishangaa kuikuta picha yake ndani mwake, ikiwa imeambatanishwa na kuku mweusi na vitu vingine.
Alisema kwamba jeneza hilo lilitelekezwa nje ya lango la kuingia kwake Usiku wa Jumamosi iliyopita na kutoa tahadhari kuu kwa yeyote ambaye yuko nyuma ya tukio hilo.
Alisema kwamba yeye haogopi chochote na yeyote huku akimtaka mhusika kuwasiliana na kampuni yake ya kutengeneza na kuuza samani kwa ajili ya kuundiwa jeneza la maana.
“Yeyote aliyedondosha jeneza hili kwenye lango langu siku ya Jumamosi usiku wa manane, nataka tu kukufahamisha kuwa siogopi vitisho vya kuuawa. Tafadhali wasiliana na Morara Home Furniture kwa jeneza bora lenye umaliziaji mzuri,” Kebaso alisema.
“Je! unajua kuwa baba yangu aliye mbinguni aliumba ubongo na mikono inayotengeneza majeneza? Ninaweza kukufanyia kuwa bora zaidi. Kuja mchana nikutengenezee jeneza safi. Acha mke wangu na familia yangu nje ya siasa,” aliongeza.
Kando na picha yake, kwenye jeneza hilo pia kulikuwa na picha ya mke wake na vitu vingine vilivyofungashwa kando na kuku mweusi aliyeonekana kutokuwa na uhai.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!