
FAITH Kathambi, mwanamke aliyegonga vichwa vya habari takribani mwezi mmoja uliopita katika kaunti ya Kisii akichapwa kwa kushukiwa kuiba unga amepata fursa nyingine ya kuishi maisha mazuri, shukrani kwa Eric Omondi.
Kathambi alikabidhiwa nyumba yake ya kifahari na mwanaharakati Eric Omondi ambaye amefanya jitihada kumjengea kupitia kwa wakfu wake wa SisiKwaSisi.
Akitoa taarifa kuhusu ujenzi huo, Eric Omondi aliwashukuru Watu wote waliochangia katika michango ya kufanikisha ujenzi wa jumba hilo ambalo alilionyesha kwenye video.
“MUNGU ANASHINDA. TEAM SISI KWA SISI Tunaweka Historia Polepole lakini Hakika. Kubadilisha maisha na Kuathiri Jumuiya. Mungu awabariki sana wanaotoa. SHUKRANI KUBWA SANA KWA @kpfcbuildershardware kwa kutoa Vifaa vyote vya kumalizia nyumba, Mungu ibariki @kpfcbuildershardware FAITH sio mmiliki wa Ardhi tu bali pia mwenye nyumba. MUNGU AWABARIKI,” Eric Omondi alisema.
Awali, Omondi aliwataarifu wafuasi wake kwenye Instagram kwamba Kathambi alikuwa pia amekabidhiwa shamba atakaloliita la kwake.
“Mabibi na Mabwana FAITH KATHAMBI rasmi ni Mmiliki wa Ardhi kwa Hisani ya SISI KWA SISI… MWENYEZI MUNGU AWABARIKI KILA ANAYECHANGIA,” Eric alisema.
Taarifa ya Kathambi kunyanyaswa na majirani kwa kudaiwa kuiba mfuko wa kilo mbili wa unga katika kijiji kimoja kaunti ya Kisii iliangaziwa na runinga ya Citizen na kuuza huzuni mwingi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, mama huyo mwenye mtoto mmoja aliyeonekana akichapwa na mwanamume mmoja kwa madai ya kuiba unga kutoka kwa mama mkwe alikuwa na tatizo la ulemavu pia.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!