Rais William Ruto kwa mara nyingine amekashifiwa kwa kutumia lugha isiyofaa kuwajibu wale waliopinga kampeni ya chanjo ya mifugo kote nchini.

Ruto aliwaita wajinga waliokosa ukomavu wa kumkabili kwa sababu hawajapata elimu ya kutosha.

Akizungumza huko Garissa mnamo Alhamisi, Rais aliwaacha wengi vinywa wazi na matamshi yake yaliyolenga wakosoaji wanaopinga chanjo ya karibu ng'ombe, mbuzi na kondoo milioni 80.

“Sasa kuna watu wengine wajinga wanatuambia tusichanje ngombe yetu tusipate soko la kitaifa. Si hiyo ni kukumbafu? Je, tumekuwa tukichanja rasilimali yetu ya zamani?” Ruto aliweka pozi.

Zaidi ya hayo, Ruto alionekana kumlenga kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, ambaye amekuwa akikosoa mpango wa serikali wa kutoa chanjo, akimwita "mtu wa ndengu.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Ndengu ni zao kuu la biashara katika eneo la Ukambani, anakotoka kiongozi huyo wa upinzani.

“Wewe unaenda kumsikiza mtu ya kupanda ndengu. ati anakuambia usichanje ng’ombe yako. yeye hana ng’ombe…hiyo ni mambo ya upumbavu na waende kabisa,” Ruto alisema.

Mkuu wa Nchi pia alielekeza lugha yake kwa wale anaodai hawana upeo au sifa za kitaaluma za kumrekebisha.

“Na mkiona wale wanalalamika ni watu sijui wamesomea wapi.Si mimi niko na PhD…si mimi naelewa nini inaendelea Kenya? Sasa mimi napata watu wako na elimu kidogo hapa wanajaribu kunifundisha, mnanifundisha kazi gani?”

Mnamo Desemba mwaka jana, Ruto alikashifiwa kwa kutumia maneno sawa na hayo kuwashambulia wakosoaji wa mpango huo ambao ulikuwa bado haujazinduliwa wakati huo.

"Mtu yeyote anayepinga chanjo ya kuondoa FMD na PPR ni wazimu, hana akili na labda ni mjinga," alisema wakati huo.