Kendrick Lamar alinyakua mataji mawili kati ya manne makubwa katika tuzo za Grammy za mwaka 2025.

Rapa Kendrick alitua ushindi wa Rekodi ya Mwaka na Wimbo wake wa "Not like US."

Kendrick Lamar alichukua kombe la Rekodi ya Mwaka wiki moja tu kabla ya onyesho lake la 'Super Bowl Halftime Show.'

Wakati akipokea tuzo hiyo, mwanamziki huyo mwenye umri wa miaka 37 alitoa ushindi kwa mji wake was Los Angeles.

"Hii ni shingo yangu, ambayo ilinishikilia tangu nilipokuwa mchanga, tangu nilipokuwa studio, nikijituma kuandika raps bora na kwa yote hayo. Siwezi kutoa shukrani za kutosha kwa maeneo haya ambayo nilizunguka tangu shule ya upili."Lamar alisema wakati wa hotuba yake ya kukubali ushindi katika uwanja wa Crypto.com Arena,

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Baada ya kuorodhesha vitongoji kadhaa vya L.A. ikiwa ni pamoja na Compton yake ya asili, Lamar -alitaja maeneo yaliyoathiriwa zaidi na moto wa hivi karibuni wa porini kama alivyotambua "watu na familia zilizoko katika Palisades na Altadena."

Kendrick ni rapa wa pili kushinda katika kitengo hicho baada ya Childish Gambino kushinda na wimbo wa "This Is America" mwaka wa 2019.

Ndani ya dakika chache, Lamar alirudi kwenye jukwaa baada ya wimbo wake wa Diss Track - ambao ambao pia ulishinda tuzo ya mwaka. wimbo ulinawiri mistari kadhaa za matukio ya huko Drake.

"Mwisho wa siku, [hakuna] kitu chenye nguvu zaidi kuliko muziki wa rap," Lamar alisema. "Sijali ni nini, sisi ni utamaduni. Ni lazima kukaa hapa na kuishi milele."

Aliendelea kutoa ujumbe kwa wasanii maarufu na wanaokuja akisema, "Natumai kwamba mutaheshimu sanaa ya mziki - hilo ndilo langu."

Kendrick Lamar Duckworth ni rapa, mtunzi wa nyimbo, na mtayarishaji wa muziki kutoka mjini Compton, California, Marekani. Mara nyingi anatajwa kuwa mmoja wa marapa wenye ushawishi mkubwa