Katika mtindo unaonekana kuwa wa mabadiliko zaidi kwa mwanamitindo na mjasiriamali Huddah Monroe, Huddah sasa ameazimia kukaa kimya na kusema kuwa hatajionyesha kwenye umma wala kukabiliana na shutuma kutoka kwa anayeaminika kuwa hasidi wake wa muda mrefu Vera Sidika.
Akizungumza kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumatano ya Januari 29,2025 Huddah alielezea kuwa analenga sana kuwa na maisha ya amani, kujikuza na kuendeleza biashara yake badala ya kujihusisha na umbea na mambo ya mitandaoni.
'Mara hii lazima upitie kwa Mungu ndio utanipata' aliandika katika ukurasa wake wa instagramu kuashiria kuwa kwa sasa hana haja na mambo ya zamani hata ukimsema vipi,akisisitiza kuwa matusi na kejeli mitanandaoni havitamshutua wala kumguza hata mshipa wa damu mwaka huu alifafanua.
"Huu mwaka hata ukinitusi ,i'll be mute Ujinga sitaki its level to this sht'' Aliandika kusisitiza hayuko tayari kujihusisha na masuala ambayo hayana maaana.
Huddah anayejulikana kwa muonekano wake wa kuvutia mitandaoni na ambaye huwa mneni sana katika mitandao amesisitiza kuwa kwa sasa kumpata itakuwa ni nadra akasema kuwa hatawakaribisha mashangingi vilabuni labda akupe mwaliko rasmi akadai kuwa mahali tu unaweza kumpata ni kwa mitandao ila akasema huko hatawavumilia walio na nia mbaya na ambao hawana la maana katika maisha yake.
Ujumbe huo ulilenga kuwapiga breki wale wote ambao wamekuwa na mazoea ya kumkejeli mitandaoni ili waweze kuvutia ufuasi mkubwa.
Kwa sasa amewaambia hadharani kuwa hawana chao wala si wa viwango vyake kwa sasa alisema kuwa ''yeyote aliyejaribu kunikejeli kwa mitandao ni mtu duni sana a low life bottom feeder trying to siphon my energy hii rich energy hampati ngoo" alikariri.
Badala ya kujihusisha na masuala ya mitandaoni Huddah amesisitiza kuwa kwa sasa analenga kuzamia na kuzingatia biashara yake ya urembo .
"Huu mwaka mtakoma my rich energy is reserved for my clients only @RICH BEAUTY" aliandika kuashiria amegura kutoka maisha ya ushindani mitandaoni hadi kwa taaaluma maalum, alikariri kuwa huu mwaka anawapa kipaumbele wateja wake peke wala si watu wa mitandoini wenye kasheshe nyingi.
Uamuzi wa Huddah Monrae kuamua kutojibu wapinzani wake mitandaoni kunajiri tu wakati ambapo hasimu wake wa jadi mtandaoni Vera Sidika alipomkosoa Huddah kwa kusema kuwa hapendelei kuzitazama programu au vipindi ambavyo vinazungumzia hali halisi ya maisha katika runinga, Sidika akisawiri usemi huo kama kejeli licha ya Huddah kuwa miongoni mwa wanamitindo ambao wameshiriki katika vipindi sampuli na hivyo anavyo vikashifu au kuvidunisha Vera akishauri kuwa aachane na watu wajivinjari wapendavyo kwa raha zao.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!