
Wanafunzi 60 wa shule ya upili ya Kalyet iliyoko Kipkelion, Kaunti ya Kericho wamelazwa katika hospitali ya Londiani kwa tuhuma za kula chakula chenye sumu.
Kulingana na msimamizi wa hospitali hiyo Dkt Collins Kipkoech, wanafunzi hao walikimbizwa hospitalini asubuhi baada ya kulalamikia kuumwa na tumbo, kuhara na kutapika.
Wanafunzi hao waliripotiwa kutumia Githeri ambayo ilishukiwa kuwa na maambukizi.
Dkt Kipkoech alisema wengi wa wanafunzi wametulia na huenda wakaruhusiwa kutoka hospitali huku wengine wakibaki kwa uangalizi zaidi.
Alisema wanafunzi hao walipatwa na ugonjwa wa kuharisha na kutapika, jambo linaloashiria kuwa huenda ni kisa cha sumu kwenye chakula.
Uongozi wa shule bado haujatoa maoni yoyote kuhusu suala hilo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!