
Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amesema kuwa Wakenya wamechoshwa na uongozi wa Rais William Ruto kwa vile hajatekeleza ahadi alizowaahidi.
Kalonzo, ambaye alikuwa akihutubia mikutano ya hadhara katika eneobunge la Dagoretti Kaskazini jijini Nairobi baada ya kuhudhuria ibada katika kanisa la Eden Gospel Trumpet Ministry, alisema maonyesho ya hivi majuzi ya hasira ya Rais ilionyesha hana ajenda ya wananchi name kwa hivyo hapaswi kupigiwa kura mwaka 2027.
Makamu huyo wa zamani wa Rais alisema kuwa Ruto anafahamu kuwa Wakenya hawatamchagua tena na ndiyo maana ameamua kuzunguka nchi nzima kufanya kampeni badala ya kukaa ofisini kwake Ikulu ya Nairobi na kuhakikisha kuwa nchi inafanya kazi, kama walivyokuwa wakifanya watangulizi wake.
“Nyote mmemwona Rais na wanasiasa wa karibu naye wakikasirika hivi majuzi tunapotaja walikofeli, wanapaswa kujua kwamba wakati wao umekwisha na wanapaswa kuwa tayari kufunganya virago na kuondoka kwani Wakenya watakuwa wakiwarudisha nyumbani wakati wa uchaguzi Mkuu ujao,” alisema Kalonzo.
Alimtaka mgombeaji wa Azimio katika jopo la mchujo wa IEBC Prof Adams Oloo kujiuzulu wadhifa wake mwingine wa mshauri wa Rais ili kuhakikisha kuwa mchakato huo hautapingwa mahakamani kwa kutozingatia matakwa ya kikatiba kwani shughuli hiyo inafaa kuharakishwa kuzuia mgogoro wa kikatiba.
Kalonzo alisema kuwa chama chake kililaumiwa hapo awali kutokana na ucheleweshaji huo lakini mahakama imejieleza katika suala hilo na kwamba wasingependa kuona Utawala wa Kenya Kwanza una sababu ya kuchelewesha mchakato wa kuunda miundo ya uchaguzi mkuu ujao.
“Tunamwomba Prof Adams Oloo atupilie mbali jukumu alilopewa na Rais Ruto kama mshauri wa Uchumi ili kutekeleza jukumu lake kama mwakilishi wa Azimio kwenye jopo la uteuzi wa IEBC kwani hakuna wakati wa kutafuta mbadala wake ili tuweze.
kuhakikisha kuwa mchakato huu unaharakishwa,” alisema Musyoka.
Alimtaka Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kuhakikisha kuwa watu wote waliotekwa nyara ambao hawajaachiliwa wanawasilishwa kwa familia zao kabla ya kufika mahakamani kama alivyoagizwa na ataongoza timu ya Mawakili wakuu nchini ili kuhakikisha haki inatendeka. inafanyika kwa walioathirika.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!