Real Madrid imeongoza kwa mapato duniani katika orodha iliyotolewa na kampuni ya Deloitte.
Timu hiyo ya Uhispania imetengeneza mapato ya euro bilioni moja ($1.04 bilioni) katika msimu mmoja wa 2023-24.
Real Madrid walikuwa wameipiku Manchester City na kurejea kileleni baada ya kuingiza mapato ya jumla ya euro milioni 831 katika msimu wa 2022-23.
Mataji matatu katika mwaka 2023-24 -- ikiwa ni pamoja na LaLiga na Ligi ya Mabingwa -- na kuongezeka kwa mapato ya siku ya mechi kufuatia kukamilika kwa kazi za ukarabati katika Uwanja wa Bernabeu ilihakikisha wanasalia juu ya orodha.
Deloitte ilisema mapato ya Real siku ya mechi yaliongezeka maradufu hadi euro milioni 248.
Ripoti hiyo pia ilisema kuwa vilabu 20 bora zaidi vilivyotengeneza mapato ulimwenguni viliweka rekodi ya euro bilioni 11.2 katika msimu wa 2023-24 kutokana na kurekodi mapato ya siku ya mechi na matangazo na biashara.
Mapato ya Real yanazidi hata yale ya City, ambao wanasalia katika nafasi ya pili kwenye orodha ya Deloitte wakiwa na euro milioni 838.
Paris St Germain (euro milioni 806), Manchester United (milioni 771) na Bayern Munich (milioni 765) zikitinga katika tano bora.
Kwa upande mwingine, klabu kama Arsenal (euro milioni 717), Borussia Dortmund (milioni 514), Newcastle United (milioni 372) na Aston Villa (milioni 310) ziliongeza mapato kwa kushiriki katika mechi mbalimbali za Ulaya.
Hata hivyo, mapato ya Barcelona yalipungua kwa euro milioni 63 katika mapato ya siku ya mechi baada ya kulazimishwa kucheza katika uwanja wa Estadi Olimpic Lluis wakati Camp Nou ikitengenezwa upya.
Lakini klabu hiyo ya Uhispania imesalia kileleni mwa orodha ya timu za wanawake kwa mwaka wa tatu mfululizo na mapato ya euro milioni 17.9, ongezeko la 26% kutoka msimu wa 2022-23.
Timu ya wanawake ya Arsenal ilitengeneza (euro milioni 17.9) ni ya pili, ikifuatiwa na Chelsea (milioni 13.4), Manchester United (milioni 10.7) na Real Madrid (milioni 10.5).
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!