Kocha mkuu wa Tusker Charles Okere anaamini huu ni msimu wao baada ya kuwalaza Bandari 1-0 ugani Kenyatta na kukwea kileleni mwa Ligi Kuu ya Kenya.

Bao la Thomas Omole lilitosha kutenganisha pande zote mbili kwenye mechi hiyo iliyokuwa na upinzani mkali.

"Nimefurahishwa na matokeo ya leo. Haya ni matokeo ya kuridhisha kwa kuzingatia asili ya wapinzani wetu. Nina furaha wachezaji walicheza kwa kufuata maelekezo katika muda wote wa mechi na tulistahili kushinda kwa tofauti kubwa," alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Okere alisema ushindi huo umeongeza matumaini yao ya kuwania taji hilo. “Sote tunatumai kufanya vyema msimu huu na tutafurahia kushinda taji la KPL huku tukiangazia kufuzu kwa mashindano ya bara,” akasema.

Kocha mkuu wa Bandari Ken Odhiambo alikiri kushindwa.

“Tulionyesha mchezo bora lakini mambo hayakwenda sawa na tulivyopanga, tumeainisha baadhi ya maeneo ambayo tunatakiwa kuyafanyia kazi kabla ya pambano letu lijalo, bado tunaamini kuwa tunakaribia sana kuwania ubingwa,” alisema.