
Vijana wanne wa Kenya waliotekwa nyara mnamo Desemba 2024 wamewasiliana na familia zao.
Mnamo Jumatatu asubuhi, familia za Bernard Kavuli, Billy Mwangi, Rony Kiplangat na Peter Muteti walisema jamaa zao walikuwa wamewasiliana nao.
Peter Muteti alipatikana Nairobi CBD, huku familia yake ikiripoti kwamba amechanganyikiwa na sasa anapata nafuu kutoka nyumbani.
Rony alipatikana katika Kaunti ya Machakos, na Bernard Kavuli, aliyetekwa nyara Ngong kupatikana Kitale.
Mchoraji katuni Kibet Bull bado hajulikani aliko. Familia hiyo inaeleza kuwa wamesikia tu kutoka kwa Rony Kiplangat, kakake Kibet ambaye alipotea kabla ya mchora katuni huyo kutekwa nyara.
Steve Mbisi, ambaye pia ameripotiwa kutoweka bado hajapatikana.
Kumekuwa na kilio cha wananchi kwa vijana hao kuachiwa huku polisi wakikanusha taarifa za kuhusika na utekaji nyara huo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!