Rais William Ruto ameionya kampuni iliyopewa kandarasi ya kukarabati uwanja wa Bukhungu akidai kuwa mradi huo unaendelea kwa kasi ndogo sana.

Maoni ya Rais yalijiri baada ya kuzuru uwanja huo wenye viti 30,000 katika Kaunti ya Kakamega.

"Kasi ambayo Uwanja wa Bukhungu unakarabatiwa haukubaliki. Uboreshaji wa uso wa kituo lazima ukamilike katikati ya 2026," alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Wizara ya michezo na kazi za umma ipo chini ya maelekezo ya kukagua hatua iliyofikiwa hadi sasa na kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati,” aliongeza.

Ruto alitoa onyo kali kwa wanakandarasi wanaochelewesha utekelezaji wa miradi muhimu ya serikali.

Rais alisema serikali imejipanga kutekeleza ahadi zake kwa wananchi, akisema wakandarasi wanaohujumu juhudi zao hawatavumiliwa.

“Kuna wakandarasi wengi wanatuangusha, na hatutawaruhusu. Huu ni mwaka wa kuwasilisha ajenda zetu kama tulivyopanga,” alisema.

Rais alitoa matamshi sawia huko Kisii, ambapo alikagua ujenzi wa Kituo cha Saratani cha Kisii. Alieleza kutoridhishwa na maendeleo ya mradi huo.

Rais Ruto alimwagiza mwanakandarasi huyo kutekeleza mradi huo kuambatana na makubaliano la sivyo akabiliane na kusitishwa kwa kandarasi hiyo.

“Umelipwa pesa zote zinazohitajika. Hakuna sababu yoyote kwa nini mradi huu hauendelei,” alisema.