Rais William Ruto amewaonya wafugaji dhidi ya kupinga mpango wa chanjo ya mifugo yao akisema hatua hiyo inalenga kuboresha mavuno yao. 

Rais aliyanena hayo mjini Kilgoris alipokutana na wenyeji na viongozi wa mashinani kutoka kaunti za Wamasai.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Ruto alisema zoezi la chanjo litakuwa la hiari wakati ugavi huo utakapoanza. Chanjo hiyo inanuiwa kuongeza mavuno ya mifugo na kuboresha ubora wa uuzaji wa nyama nje ya nchi.

Rais alisema kuwa kupinga chanjo hiyo kutahatarisha uuzwaji wa nyama uliopangwa. Rais aliwaambia wakazi wa Narok kwamba Gavana wa Narok Patrick Ole Ntutu, pamoja na serikali ya kitaifa, wamezindua kiwanda cha pamoja cha kusindika nyama kusafirisha nyama nje ya nchi.

“Hapa Narok, gavana wenu ametafuta marafiki wanaleta pesa na pia sisi, national government tunaleta pesa ili muwe na kiwanda kikubwa zaidi cha kusindika nyama hapa Narok ya kuuza nyama yenu nje. Mnataka kuuza bidhaa iliyo gonjwa?” aliuliza Ruto.

   Aidha aliwaambia wakazi wa Narok kwamba utoaji wa chanjo utakuwa wa hiari. “Itakuwa hiari. Ukitaka, sawa. Kama hutaki, shauri yako,” Ruto aliongeza.