Mtoto wa kike mwenye umri wa miezi sita anapigania maisha yake katika hospitali ya kaunti ndogo ya Yala baada ya kuchomwa na kujeruhiwa vibaya na babake kufuatia mzozo wa nyumbani katika kijiji cha Siandha ‘B’ eneo la East Gem.

Babake mtoto huyo ambaye ametambuliwa kama Victor Njeri anasemekana kuwa na ugomvi wa kinyumbani na mkewe alipoamua kumwagia mtoto huyo maji ya moto.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kisa hicho kiliripotiwa kwa kituo cha polisi cha Ramula na kaimu Msaidizi wa Chifu Vitalis Otunga, ambaye alieleza kuwa mwanamume huyo alitaka kumwagia maji ya moto mke aliyekuwa amembeba mtoto.

Kufuatia tukio hilo, mama wa mtoto huyo alipiga kelele, na kuvutia hisia za majirani, ambao walikimbilia eneo la tukio na kumpeleka mtoto hospitali.

Majirani hao walimshukia mhalifu huyo kwa mateke na vipigo kabla ya kuokolewa na maafisa wa kituo cha polisi cha Ramula.

Mtoto na baba wanaendelea na matibabu katika hospitali moja huku uchunguzi ukiendelea kuhusu suala hilo.