Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua alilazimika kukimbilia usalama wake baada ya kurushiwa vitoa machozi mita chache kutoka alipokuwa ameketi na viongozi wengine. 

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Gachagua alikuwa akihudhuria hafla ya kutoa shukrani kwa mwakilishi wa wadi ya Shamata Gitau Njamba huko Nyandarua. Vurugu hizo ziliwaacha watu kadhaa kujeruhiwa huku polisi wakizidiwa nguvu na umati huo wenye hasira. 

Kisa hicho kilitokea wakati Seneta wa Nyandarua John Methu alipokuwa akitoa hotuba yake. Viongozi wa kidini pia hawakusalimika katika vurugu hizo.

Mshukiwa mkuu aliyefungwa pingu na polisi anayedaiwa kuwa afisa wa polisi aliyevalia kiraia alisema alirusha kopo hilo.

“Huwezi kutawala watu kwa nguvu na wala huwezi kuwalazimisha kufanya unavyotaka... tutazungumza nao na kujua ni nini kiliwakasirisha...,” alisema Gachagua.

Ikiwa imepita mwezi mzima tangu Gachagua kushambuliwa mjini Limuru wakati wa hafla ya maziko, na kufichua ongezeko la joto la kisiasa na kutovumiliana nchini.

Gachagua anadai shida zake zimepangwa vyema na Serikali. “Ima ukivunja mkutano au ukiwatuma vijana waje na visu hivi, watu wote tayari wameondoka UDA,” aliongeza Gachagua. Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo ili kujua kiini cha shambulio hilo.