MALKIA wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Nandy amefichua kiasi cha peza alizopokea baada ya kutumbuiza kwa muda mfupi zaidi katika hafla moja ya harusi ya kikwasi jijini Mombasa.


Nandy alikuwa miongoni mwa wasanii maarufu walioalikwa kutumbuiza katika harusi hiyo iliyofanyika Jumamosi Desemba 21 katika jiji la Mombasa.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Nandy alitumbuiza kwa dakika 10 pekee na kufichua kwamba dakika zake kumi zilimuingizia jumla ya dola laki tatu na nusu, sawa na shilingi milioni 45 pesa za Kenya.


“Kulipwa jumla ya dola 350k [Ksh 45m] baada ya kutumbuiza kwa dakika 10 tu sio mchezo wa kitoto,” Nandy alifichua.


Katika hafla hiyo, rais Ruto alionekana akizungumza na wahudhuriaji huku akiwa amevalia joho la Kiislamu, ishara tosha kwamba ilikuwa harusi ya dini ya Kiislamu.


Inaarifiwa kwamba msanii Diamond Platnumz pia alikuwepo jijini Mombasa Jumamosi, alikohudhuriaq kwa muda kabla ya kurudi Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa albamu mpya ya msanii na mpenzi wake, Zuchu.


Ujio wa Duiamond nchini Kenya ulijiri wiki chache tu baada ya shoo yake jijini Nairobi kutibuka kwa kile alichokitaja kuwa ni waandaaji kukosa kukidhi vigezo vya usalama wake kama msanii.


Diamond alitarajiwa kutumbuiza katika hafla hiyo ya Desemba 7 kama msanii mkuu katika tamasha la Furaha Festival lakini alishindwa kutyumbuiza baada ya zogo kuzuka katika usiku huo wa tafrija.


Baadae, kuliibuka uvumi kwamba Willy Paul alifarakana na uongozi wa Diamond kuhusu ni nani wa kuingia jukwaani kwanza, vita ambayo Pozee alishinda na Diamond kuondoka bila kuwatumbuizia mashabiki wake.


Diamond baadae alifichua kwamba alipokea zaidi ya shilingi milioni 19 japo hakutumbuiza na kusema kwamba kwa mujibu wa mkataba wake, asingerudisha hela hizo.


Ufichuzi wa Nandy kulipwa zaidi ya milioni 45 za Kenya kwa dakika 120 unasibua maswali kuhusu Sanaa ya humu nchini ambapo baadhi ya wasanii wanalipwa kutumbuiza au kutokea katika hafla mbalimbali.


Baadhi wanahisi kiasi kikubwa wanacholipwa wasanii wa kigeni ni kengele ya kuwagutusha kutoka usingizi wasanii wa humu nchini kujua jinsi ya kuinadi Sanaa yao kwa niia ya kitaaluma zaidi.