Siku ya Ijumaa jioni, winga wa Manchester United Amad Diallo alithibitisha kuwa ana uhusiano mzuri na mwenzake Rasmus Hojlund baada ya mzozo wao mdogo mnamo Alhamisi usiku.
Wachezaji hao wawili walionekana kutofautiana na kurushiana cheche za maneno makali uwanjani baada ya mechi yao ya Europa dhidi ya Viktoria Plzen Alhamisi usiku.
Siku
moja baadaye, Amad Diallo alichapisha picha nzuri yake na Hojlund wakisalimiana
kwenye uwanja wa Plzen na kuisindikiza kwa emoji za upendo na amani.
Hii ilionekana kuthibitisha kuwa wawili hao waliendelea kusuluhisha mzozo wao baada ya kisa cha kushangaza kilichotokea mjini Plzen katika Jamhuri ya Czech.
Diallo na Hojlund walionekana kuhusika katika mzozo na kurushiana cheche za maneno ya hasira baada ya mechi ya Alhamisi usiku.
Mashetani Wekundu walishinda 2-1 katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Doosan Arena nchini Jamhuri ya Czech.
Hojlund ambaye aliingia uwanjani kama mchezaji wa akiba katika dakika ya 56 alifunga mabao mawili na angeweza kusaidiwa kwa nafasi ya kufunga hat-trick na Diallo katika dakika za mwisho.
Hata hivyo, winga huyo kutoka Ivory Coast hakumpata mwenzake kwa pasi lake.
Viktoria ambao walikuwa nyuma kwa mabao 2-1 kutoka dakika ya 62 walikuwa wakisonga mbele nyakati nyingi wakitafuta bao la kusawazisha, ambalo liliunda nafasi kwa kaunta za United.
Kwenye moja ya kaunti zake katika dakika ya mwisho, Hojlund aliamua kukaa na mpira na kutompea pasi mwenzake yeyote.
Matukio yaliyotokea katika dakika za mwisho za mechi yaliwafanya Hojlund na Diallo kuwa na majibizano ya maneno makali baada ya mchuano.
Alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo baada ya mechi, meneja wa Manchester United, Ruben Amorin alisema anaamini ilikuwa ni ishara nzuri sana ya wachezaji wawili wanaojali kushinda.
Amorim alilinganisha mzozo kidogo kati ya washambuliaji hao wawili na kutoelewana kwa familia ambako kunaweza kueleweka kwa urahisi.
"Tunahitaji kuhisi kitu. Ikiwa tunahitaji kupigana kila mmoja, ni kama familia. Usipojali, hufanyi chochote. Unapojali - unapigana na kaka yako, na mama yako, baba yako," Amorim alisema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!