Mtangazaji maarufu wa Injili Joyce Gituro amemkaribisha rasmi mfanyibiashara Sarah Njoki Nyaga almaarufu Sarah Kabu katika maisha bila mume.
Akiongea kwenye taarifa ya video ambayo alichapisha Jumamosi, Bi Gituro alidokeza baadhi ya mambo ambayo Sarah anafaa kutarajia katika maisha yake mapya.
Alizungumza kuhusu jinsi kuna hukumu nyingi na matusi na baada ya talaka na akamtaka mfanyibiashara huyo afanye kazi katika kuboresha maisha yake.
“Vipi Sarah Kabu, karibu kwa upande huu mwingine. Nakujua wewe ni mwanamke mchapakazi sana. Upande huu mwingine, utahukumiwa, utanyanyaswa kweli. Anza kujuana na mekanika wa kupelekea gari, anza kujua kuweka balbu. Fanya kazi kwa bidii, Watoto wako watahukumiwa lakini utakuwa na amani tele,” Bi Gituro aliambia Sarah kwenye video.
Mtangazaji huyo wa zamani wa redio aliendelea kumshauri Sarah asisite kurudi kwa mumewe ikiwa kuna wakati atakaposhawishika kufanya hivyo.
Pia alimshauri mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Bonfire Adventures kukoma kuzungumzia baba wa watoto wake wawili, Simon Kabu.
"Kufikia sasa, acha kumjadili ex wako, zingatia kazi yako na biashara. Zingatia kujiboresha. Fanya kazi kwa bidii sana. Karibu tena kwa upande huu mwingine. Huku huwa tunatukanwa tu bure lakini tuna furaha,” alisema.
Katika mahojiano ya hivi majuzi, Sarah alithibitisha kuwa yuko mbioni kutengana rasmi na mumewe wa miaka mingi na mshirika wa kibiashara Simon Kabu.
Akizungumzia mipango yake inayofuata baada ya kumalizika kwa ndoa yake, alithibitisha kwamba anapanga kuolewa tena katika siku zijazo.
Mfanyibiashara huyo mwenye umri wa miaka 46 alibainisha kuwa hajui jinsi ya kuwa katika uchumba kwani alilelewa kuwa mke.
“Mimi ata sijui nataka nini. Sina uhakika kama nataka kuchumbiwa tena. Lakini ninachojua ni kwamba nataka kuolewa tena,” Sarah alisema.
“Nimelelewa kuwa mke hivyo sijui maisha nikiwa mtaani, nikiwa
single. Kwangu sijui hatua hiyo ya kuchumbiwa,” aliongeza.
Mama huyo wa watoto wawili alifichua kuwa kwa sasa yuko katika
harakati za kupona kufuatia kuisha kwa ndoa yake ya miaka mingi.
"Ikiwa una mawazo ya jinsi mtu anaweza kupona kutokana na mshtuko wa moyo, ebu niambieni njia ya kupona. Mimi kwa sasa napona. Nadhani sasa ndio napata ukweli baada ya mambo kujulikana wazi,” alisema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!