Nchi ya Mauritius imeihakikishia Kenya kura yake kwa mgombea uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Raila Odinga kabla ya uchaguzi wa Februari 2025.
Raila ameacha kujihusisha na siasa
za humu nchini ili kutafuta nafasi hiyo yenye ushawishi mkubwa lakini
anakabiliwa na ushindani mkali katika azma yake ya kumrithi Moussa Faki Mahamat
wa Chad ambaye muhula wake utafikia kikomo.
Siku ya Jumanne, Rais William Ruto alisema alizungumza na Waziri Mkuu mteule wa Mauritius ambaye alimpa ahadi yake kwamba nchi hiyo ya kisiwa itampigia kura Raila.
Maneno ya kuunga mkono Kenya yanaashiria kuwa Anil Kumarsingh Gayan ambaye mgombeaji kutoka Mauritius amejiondoa katika kinyang'anyiro hicho amejiondoa.
"Nimefanya mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu mteule wa Mauritius, Mhe Navinchandra Ramgoolam. Nilimpongeza kwa kuchaguliwa kwake na kwa imani ambayo watu wa nchi yake wameonyesha kwake na chama chake," Ruto alisema kwenye X.
"Tulithibitisha uhusiano mkubwa na mzuri wa kidiplomasia kati ya nchi zetu mbili na watu na tukajitolea kuimarisha uhusiano huo. Waziri Mkuu Ramgloolam alithibitisha kumuunga mkono mgombeaji wa Kenya kwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mhe Raila Odinga."
Mauritius ni nchi ya kisiwa katika Bahari ya Hindi, iko karibu na pwani ya kusini mashariki mwa Afrika, mashariki mwa Madagaska.
Kuidhinishwa kwa Raila nchini humo kunamaanisha kuwa kinyang'anyiro hicho sasa kimepungua hadi kufikia wagombea watatu pekee - Raila, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Djibouti Mahamoud Ali Youssouf na Richard Randriamandrato wa Madagascar.
Raila anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Youssouf ambaye wachanganuzi wanasema anafurahia sapoti nzuri kutoka kwa nchi zinazozungumza Kifaransa.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!