Meneja wa Manchester City Pep Guardiola alitokea kwenye vyombo vya habari akiwa na michubuko mingi usoni kufuatia mechi kali dhidi ya Feyenoord Jumanne usiku.

City walikuwa wameanza mechi vizuri na tayari walikuwa wanaongoza 3-0 katika dakika ya 74 kabla ya Feyonoord kufunga mabao 3 kati ya dakika ya 75 na ya 89.

Kufikia mwisho wa mechi, kocha Guardiola alikuwa na michubuko kadhaa usoni na aliulizwa aliipataje.

“Nilipata mikato kwa kidole changu, (nilijikwaruza) kwa kucha. Nataka kujiumiza,” Guardiola alisema kwa utani kabla ya kuwaaga wanahabari.

Akizungumzia mechi hiyo ya kusikitisha kwao, Guardiola alikiri kwamba imani ya wachezaji wake ilikuwa chini baada ya kutupilia mbali uongozi wa bao tatu zikiwa zimesalia dakika 15 tu na kuruhusu sare ya 3-3 nyumbani dhidi ya Feyenoord kwenye Mchuano wa Ligi ya Mabingwa.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kufikia dakika ya 74, City walikuwa wanaelekea kupata ushindi baada ya kuongoza kwa mabao matatu huku mshambulizi Erling Haaland akiwa amefunga mabao mawili.

Hata hivyo, wageni wao walishangaza kwa kufunga mabao matatu katika robo ya mwisho ya saa – ikiwa ni mara ya kwanza walipotupilia mbali uongozi kama huo chini ya Guardiola - na kuwaacha washindi wa Ligi ya Mabingwa 2023 wakiwa katika nafasi ya 15 katika mfumo mpya baada ya mechi ya sita.

"Tulipoteza michezo mingi hivi majuzi, sisi ni dhaifu na bila shaka, tunahitaji ushindi," aliiambia wanahabari baada ya mechi.

"Kila mtu anaijua hali ilivyo; hatutakiwi kuzoea chochote. Kesho [Jumatano], tunapaswa kufanya mazoezi, kupona kisha kuandaa mchezo unaofuata. Tuna siku mbili au tatu za kujiandaa na hilo na kulikabili. Tutajifunza kwa siku zijazo.

"Umekuwa msimu mgumu sana kwetu kwa mazingira mengi na leo, kwa bahati mbaya, mchezo ulifanyika vizuri, tuliwaadhibu katika muda sahihi. Timu ilikuwa imejitolea kwa mambo mengi. Lakini kwa bahati mbaya, kitu kilifanyika na tulikuwa hatuna nguvu za kutosha. Tunapaswa kuepuka makosa haya," Guardiola alisema.

Sare ya Jumanne ilikua mechi ya sita mfululizo kwa Man City bila ushindi.